Logotipo da YouVersion
Ícone de Pesquisa

Zaburi 3

3
Mwamini Mungu katika dhiki
Zaburi ya Daudi alipomkimbia mwanawe, Absalomu.
1 # 2 Sam 15:13—17:22 BWANA, watesi wangu wamezidi kuwa wengi,
Ni wengi wanaonishambulia,
2 # 2 Sam 16:8; Zab 22:7,8 Ni wengi wanaoiambia nafsi yangu,
Hana wokovu huyu kwa Mungu.
3 # 2 Fal 25:27; Zab 27:6 Lakini Wewe, BWANA, U ngao yangu pande zote,
Utukufu wangu na mwinua kichwa changu.
4Kwa sauti yangu namwita BWANA
Naye aniitikia toka mlima wake mtakatifu.
5 # Zab 4:8; Mit 3:24; Mdo 12:6 Nilijilaza na kulala usingizi, kisha ninaamka tena,
Kwa kuwa BWANA ananitegemeza.
6Sitayaogopa maelfu na maelfu ya watu,
Waliojipanga Juu yangu pande zote.
7BWANA, uinuke, Mungu wangu, uniokoe,
Maana umewapiga taya adui zangu wote;
Umewavunja meno wasio haki.
8 # Zab 37:39,40; Mit 21:31; Hes 13:4 Wokovu ni wa BWANA;
Baraka yako na iwe juu ya watu wako.

Atualmente Selecionado:

Zaburi 3: SRUV

Destaque

Compartilhar

Copiar

None

Quer salvar seus destaques em todos os seus dispositivos? Cadastre-se ou faça o login