Logotipo da YouVersion
Ícone de Pesquisa

Zaburi 11

11
Wimbo wa kumtumainia Mungu
Kwa mwimbishaji. Ya Daudi.
1BWANA ndiye niliyemkimbilia.
Mbona mnaiambia nafsi yangu,
Kimbia kama ndege mlimani kwenu?
2Maana, tazama, wasio haki wanaupinda uta,
Wanaitia mishale yao katika upote,
Ili kuwapiga gizani wanyofu wa moyo.
3Kama misingi ikiharibika,
Mwenye haki atafanya nini?
4 # Hab 2:20; Efe 5:13; Ebr 4:13 BWANA yu katika hekalu lake takatifu.
BWANA ambaye kiti chake kiko mbinguni,
Macho yake yanaangalia;
Kope zake zinawapima wanadamu.
5 # Ayu 5:17; Zab 94:12 BWANA humjaribu mwenye haki;
Bali nafsi yake humchukia asiye haki,
Na mwenye kupenda udhalimu.
6Awanyeshee wasio haki mitego,
Moto na kiberiti na upepo wa joto
Na viwe fungu la kikombe chao.
7Kwa kuwa BWANA ni mwenye haki,
Apenda matendo ya haki,
Wanyofu wa moyo watauona uso wake.

Atualmente Selecionado:

Zaburi 11: SRUV

Destaque

Compartilhar

Copiar

None

Quer salvar seus destaques em todos os seus dispositivos? Cadastre-se ou faça o login