1
Luka MT. 8:15
New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921
Nazo penye udongo mwema, hawa ndio ambao kwamba kwa moyo mzuri na mwema hulisikia neno, wakalishika, wakazaa kwa saburi.
Compare
Luka MT. 8:15ਪੜਚੋਲ ਕਰੋ
2
Luka MT. 8:14
Nazo zilizoangukia miibani, hawa ndio waliosikia, nao wakienda zao husongwa na shughuli, na mali, na anasa za maisha, wasizae kwa utimilifu.
Luka MT. 8:14ਪੜਚੋਲ ਕਰੋ
3
Luka MT. 8:13
Na wale juu ya mwamba ndio wale ambao, walisikiapo neno, hulipokea kwa furaha; na hawa hawana mizizi, huamini kwa kitambo, na wakati wa kujaribiwa hujitenga.
Luka MT. 8:13ਪੜਚੋਲ ਕਰੋ
4
Luka MT. 8:25
Akawaambia, Imani yenu iko wapi? Wakaogopa, wakastaajabu, wakasemezana, Huyu ni nani, bassi, kwa kuwa hatta upepo na bahari aviamuru vikamtii?
Luka MT. 8:25ਪੜਚੋਲ ਕਰੋ
5
Luka MT. 8:12
Na wale wa njiani, ndio wasikiao, ndipo huja Shetani na kulitoa lile neno mioyoni mwao, illi wasije wakaamini, wakaokoka.
Luka MT. 8:12ਪੜਚੋਲ ਕਰੋ
6
Luka MT. 8:17
Kwa maana hakuna neno lililostirika ambalo halitakuwa dhabiri, wala neno lililofichwa ambalo halitajulikana, na kutokea wazi.
Luka MT. 8:17ਪੜਚੋਲ ਕਰੋ
7
Luka MT. 8:47-48
Yule mwanamke alipoona ya kuwa hakustirika, akaja akitetemeka, akamwangukia, akamweleza mbele ya watu wote sababu hatta akamgusa, na jinsi alivyoponywa marra moja. Akamwambia. Jipe moyo mkuu, binti, imani yako imekuponya; enenda zako kwa amani.
Luka MT. 8:47-48ਪੜਚੋਲ ਕਰੋ
8
Luka MT. 8:24
Wakamwendea, wakamwamsha, wakisema, Mwalimu, Mwalimu, tunaangamia. Akaondoka, akaukemea upepo, na msukosuko wa maji, vikakoma, kukawa shwari.
Luka MT. 8:24ਪੜਚੋਲ ਕਰੋ
Home
ਬਾਈਬਲ
Plans
ਵੀਡੀਓ