Ndipo, baba yake Isaka alipomwitikia na kumwambia:
Tazama! Hapo, utakapokaa,
manono ya nchi yatakuwa mbali,
nao umande wa mbinguni juu.
Utajilisha mapato ya upanga wako,
utamtumikia ndugu yako;
lakini itakuwa, ukijikaza utalivunja kongwa,
litoke shingoni pako!