1
Yohana 13:34-35
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
“Nawapa amri mpya: Pendaneni ninyi kwa ninyi. Mnapaswa kupendana kama mimi nilivyowapenda ninyi. Endapo mtapendana ninyi kwa ninyi watu wote watatambua kuwa ninyi ni wafuasi wangu.”
ប្រៀបធៀប
រុករក Yohana 13:34-35
2
Yohana 13:14-15
Mimi ni Bwana na Mwalimu wenu. Lakini niliwaosha miguu yenu kama mtumishi. Hivyo nanyi mnapaswa kuoshana miguu yenu. Nilifanya hivyo kama mfano. Hivyo nanyi mnapaswa kuhudumiana ninyi kwa ninyi kama nilivyowahudumia.
រុករក Yohana 13:14-15
3
Yohana 13:7
Yesu akamjibu, “Huyaelewi ninayofanya hivi sasa. Lakini utayaelewa baadaye.”
រុករក Yohana 13:7
4
Yohana 13:16
Mniamini mimi, watumishi huwa sio wakubwa kuzidi bwana zao. Wale waliotumwa kufanya jambo fulani sio wakubwa kumzidi yule aliyewatuma.
រុករក Yohana 13:16
5
Yohana 13:17
Sasa, mkielewa maana ya yale niliyotenda, Mungu atawabariki mkiyatendea kazi.
រុករក Yohana 13:17
6
Yohana 13:4-5
Kwa hiyo walipokuwa wakila, Yesu alisimama na kulivua vazi lake. Akachukua taulo na kuifunga kiunoni mwake. Kisha akamimina maji katika bakuli na kuanza kuwaosha miguu wafuasi wake. Kisha akaifuta miguu yao kwa taulo aliolifunga kiunoni mwake.
រុករក Yohana 13:4-5
គេហ៍
ព្រះគម្ពីរ
គម្រោងអាន
វីដេអូ