1
Yohana 12:26
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
Kama mtu atanitumikia inampasa anifuate. Watumishi wangu watakuwa pamoja nami popote nitakapokuwa. Mtu atakayenitumikia Baba yangu atamheshimu.
ប្រៀបធៀប
រុករក Yohana 12:26
2
Yohana 12:25
Yeyote anayeyapenda maisha yake aliyonayo atayapoteza. Yeyote atakayetoa maisha yake kwa Yesu katika ulimwengu huu atayatunza. Nao wataupata uzima wa milele.
រុករក Yohana 12:25
3
Yohana 12:24
Ni ukweli kwamba mbegu ya ngano inapaswa kuanguka katika ardhi na kuoza kabla ya kukua na kuzaa nafaka nyingi ya ngano. Kama haitakufa, haitaongezeka zaidi ya hiyo mbegu moja.
រុករក Yohana 12:24
4
Yohana 12:46
Nimekuja katika ulimwengu huu kama mwanga. Nimekuja ili kila mmoja atakayeniamini asiendelee kuishi katika giza.
រុករក Yohana 12:46
5
Yohana 12:47
Sikuja ulimwenguni humu kuwahukumu watu. Nimekuja ili kuwaokoa watu wa ulimwengu huu. Hivyo mimi siye ninayewahukumu wale wanaosikia mafundisho yangu bila kuyafuata.
រុករក Yohana 12:47
6
Yohana 12:3
Mariamu akaleta manukato ya thamani sana yaliyotengenezwa kwa nardo asilia kwenye chombo chenye ujazo wa nusu lita hivi. Akayamwaga manukato hayo miguuni mwa Yesu. Kisha akaanza kuifuta miguu ya Yesu kwa nywele zake. Harufu nzuri ya manukato hayo ikajaa nyumba nzima.
រុករក Yohana 12:3
7
Yohana 12:13
Hawa walibeba matawi ya miti ya mitende na kwenda kumlaki Yesu. Pia walipiga kelele wakisema, “‘Msifuni Yeye!’ ‘Karibu! Mungu ambariki yeye anayekuja kwa jina la Bwana!’ Mungu ambariki Mfalme wa Israeli!”
រុករក Yohana 12:13
8
Yohana 12:23
Yesu akawaambia Filipo na Andrea, “Wakati umefika kwa Mwana wa Adamu kuupokea utukufu wake.
រុករក Yohana 12:23
គេហ៍
ព្រះគម្ពីរ
គម្រោងអាន
វីដេអូ