Akara Njirimara YouVersion
Akara Eji Eme Ọchịchọ

Mwanzo UTANGULIZI

UTANGULIZI
Kitabu cha Mwanzo ndicho cha kwanza katika orodha ya vitabu vya Biblia. Jina Mwanzo linatokana na kitabu chenyewe (1:1) kwa maana ya asili na chanzo cha ulimwengu, mtu, dhambi, kifo na taifa la Israeli. Jambo la msingi ni Mungu na mtu katika uhusiano wao na pia mpango wa Mungu wa wokovu na uteule wa watu wa wake.
Mungu ndiye Muumba wa vitu vyote. Mungu alimwumba mwanadamu, lakini mwanadamu huyo alimwasi Muumba wake, na kwa uasi wake watu wote wakawa wenye dhambi. Matokeo ya dhambi yakawa kifo. Kwa kuwa tangu mwanzo Mungu aliahidi kuujalia uumbaji wake baraka zake. Ndipo hata mtu alipoasi, Mungu aliendelea kujifunua kwake, kunena na wateule wake, kuwapa wajibu na kuwabariki.
Yaliyomo:
1. Simulizi la awali kuhusu ulimwengu na mtu, Sura 1–11
(a) Kuumba ulimwengu (1–2)
(b) Uasi na kuanguka kwa mtu (3)
(c) Uasi unaongezeka (4–5)
(d) Nuhu na gharika (6–9)
(e) Mnara wa Babeli (10–11)
2. Historia ya awali ya Waisraeli, Sura 12–50
(a) Habari za Abrahamu na watoto wake (12–24)
(b) Habari za Yakobo (25–36)
(c) Habari za Yusufu (37–50)

Nke Ahọpụtara Ugbu A:

Mwanzo UTANGULIZI: RSUVDC

Mee ka ọ bụrụ isi

Kesaa

Mapịa

None

Ịchọrọ ka echekwaara gị ihe ndị gasị ị mere ka ha pụta ìhè ná ngwaọrụ gị niile? Debanye aha gị ma ọ bụ mee mbanye