1
Lk 13:24
Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia
Jitahidini kuingia katika mlango ulio mwembamba, kwa maana nawaambia ya kwamba wengi watataka kuingia, wasiweze.
Lee anya n'etiti ihe abụọ
Nyochaa Lk 13:24
2
Lk 13:11-12
Na tazama, palikuwa na mwanamke aliyekuwa na pepo wa udhaifu muda wa miaka kumi na minane, naye amepindana, hawezi kujinyosha kabisa. Yesu alipomwona alimwita, akamwambia, Mama, umefunguliwa katika udhaifu wako.
Nyochaa Lk 13:11-12
3
Lk 13:13
Akaweka mikono yake juu yake, naye akanyoka mara hiyo, akamtukuza Mungu.
Nyochaa Lk 13:13
4
Lk 13:30
Na tazama, wako walio wa mwisho watakaokuwa wa kwanza, na wa kwanza watakaokuwa wa mwisho.
Nyochaa Lk 13:30
5
Lk 13:25
Wakati mwenye nyumba atakaposimama na kuufunga mlango, nanyi mkaanza kusimama nje na kuubisha mlango, mkisema, Ee Bwana, tufungulie; yeye atajibu na kuwaambia, Siwajui mtokako
Nyochaa Lk 13:25
6
Lk 13:5
Nawaambia, Sivyo; lakini msipotubu, ninyi nyote mtaangamia vivyo hivyo.
Nyochaa Lk 13:5
7
Lk 13:27
Naye atasema, Nawaambia, Siwajui mtokako; ondokeni kwangu ninyi nyote mlio wafanyaji wa udhalimu.
Nyochaa Lk 13:27
8
Lk 13:18-19
Kisha alisema, Ufalme wa Mungu umefanana na nini? Nami niufananishe na nini? Umefanana na punje ya haradali aliyotwaa mtu akaitupa katika shamba lake; ikamea, ikawa mti; ndege wa angani wakakaa katika matawi yake.
Nyochaa Lk 13:18-19
Ebe Mmepe Nke Mbụ Nke Ngwá
Akwụkwọ Nsọ
Atụmatụ Ihe Ogụgụ Gasị
Vidiyo Gasị