Mattayo MT. 1
1
1KITABU eba ukoo wa Yesu Kristo, mwana wa Daud, mwana wa Ibrahimu. 2Ibrahimu alimzaa Isaak; Isaak akamzaa Yakob; Yakob akamzaa Yuda na ndugu zake; 3Yuda na Tamar wakamzaa Parez na Zara; Parez akamzaa Esrom; Esrom akamzaa Aram; 4Aram akamzaa Aminadab; Aminadab akamzaa Nahashon; Nahashon akamzaa Salmon; 5Salmon na Rahab wakamzaa Boaz; Boaz na Ruth wakamzaa Obed; Obed akamzaa Yese; 6Yese akamzaa mfalme Daud.
Mfalme Daud na mke wa Uria wakamzaa Suleman; 7Suleman akamzaa Rehoboam; Rehoboam akamzaa Abia; Abia akamzaa Asa; 8Asa akamzaa Yehoshafat; Yehoshafat akamzaa Yoram; Yoram akamzaa Uzia; 9Uzia akamzaa Yotham; Yotham akamzaa Ahaz; Ahaz akamzaa Hezekia; 10Hezekia akamzaa Manasse; Manasse akamzaa Amon; Amon akamzaa Yosia; 11Yosia akamzaa Yekonia na ndugu zake, wakati wa uhamisho wa Babel.
12Na haada ya uhamisho ule wa Babel, Yekonia akamzaa Shealtiel; Shealtiel akamzaa Zerubbabel; 13Zerubbabel akamzaa Ahihud; Ahihud akamzaa Eliakim; Eliakim akamzaa Azor; 14Azor akamzaa Sadok; Sadok akamzaa Ahim; Ahim akamzaa Eliud; 15Eliud akamzaa Eleazar; Eleazar akamzaa Mattan; Mattan akamzaa Yakob; 16Yakob akamzaa Yusuf mumewe Mariamu aliyemzaa YESU aitwae Kristo. 17Bassi vizazi vyote tangu Ibrahimu hatta Daud vizazi kumi na vine; na tangu Daud hatta uhamisho ule wa Babel vizazi kumi na vine; na tangu uhamisho ule wa Babel hatta Kristo vizazi kumi na vine.
18Na kuzaliwa kwake Yesu Kristo kulikuwa hivi. Mariamu mama yake alipoposwa na Yusuf, kabla hawajakaribiana, alionekana ana mimba kwa uweza wa Roho Mtakatifu. 19Nae Yusuf, mumewe, kwa kuwa mtu wa haki, asitake kumwaibisha, aliazimu kumwacha kwa siri. 20Alipokuwa akifikiri haya, malaika wa Bwana akamtokea katika udoto, akisema, Yusuf, mwana wa Daud, usikhofu kumchukua Mariamu mke wako, maana mimba yake ni kwa uweza wa Roho Mtakatifu. 21Nae atazaa mtoto mwanamume, nawe utamwita jina lake Yesu, maana, ndiye atakaewaokoa watu wake na dhambi zao.
22Haya yote yamekuwa, illi litimie neno lililonenwa na Bwana kwa ujumbe wa nabii akinena,
23Angalia, mwanamke bikira atachukua mimba, nae atazaa mwana,
Na watamwita jina lake Immanuel;
tafsiri yake, Mungu kati yetu. 24Yusuf alipoamka katika usingizi, akatenda kama malaika wa Bwana alivyomwagiza; 25akamchukua mkewe; asimjue kamwe hatta alipomzaa mwanawe wa kifungua mimba; akainwita jina lake YESU.
Արդեն Ընտրված.
Mattayo MT. 1: SWZZB1921
Ընդգծել
Կիսվել
Պատճենել
Ցանկանու՞մ եք պահպանել ձեր նշումները ձեր բոլոր սարքերում: Գրանցվեք կամ մուտք գործեք
Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.