1 The 4
4
Maisha Yampendezayo Mungu
1 #
2 The 3:6
Iliyobaki, ndugu, tunakusihini na kuwaonya kwamba mwenende katika Bwana Yesu; kama mlivyopokea kwetu jinsi iwapasavyo kuenenda na kumpendeza Mungu, kama nanyi mnavyoenenda, vivyo hivyo mpate kuzidi sana. 2Kwa kuwa mnajua ni maagizo gani tuliyowapa kwa Bwana Yesu. 3#1 The 5:23; Ebr 10:10; 1 Pet 1:16Maana haya ndiyo mapenzi ya Mungu, kutakaswa kwenu, mwepukane na uasherati; 4#1 Kor 6:13,15kila mmoja wenu ajue kuuweza mwili wake katika utakatifu na heshima; 5#Yer 10:25; Zab 79:6si katika hali ya tamaa mbaya, kama Mataifa wasiomjua Mungu. 6#Zab 94:2Mtu asimpunje ndugu yake wala kumkosa katika jambo hili; kwa sababu Bwana ndiye alipizaye kisasi cha haya yote; kama tulivyowaambia kwanza, tukashuhudia sana. 7#2 The 2:13,14Maana Mungu hakutuitia uchafu, bali tuwe katika utakaso. 8#Lk 10:16; Eze 36:27; 37:14Basi yeye anayekataa, hakatai mwanadamu bali Mungu, anayewapa ninyi Roho wake Mtakatifu.
9 #
Yn 13:34; Yer 31:33,34 Katika habari ya upendano, hamna haja niwaandikie; maana ninyi wenyewe mmefundishwa na Mungu kupendana. 10#2 The 3:4Kwa maana mnafanya neno hili kwa ndugu wote walio katika Makedonia yote. Lakini twawasihi, ndugu, mzidi sana. 11#Efe 4:28; 2 The 3:8,12Tena mjitahidi kutulia, na kutenda shughuli zenu, na kufanya kazi kwa mikono yenu wenyewe, kama tulivyowaagiza; 12#Kol 4:5; 1 Kor 5:12,13ili mwenende kwa adabu mbele yao walio nje, wala msiwe na haja ya kitu cho chote.
Kuja kwa Bwana
13 #
1 Kor 15:20; Efe 2:12 Lakini, ndugu, hatutaki msijue habari zao waliolala mauti, msije mkahuzunika kama na wengine wasio na matumaini. 14#Rum 14:9; 1 Kor 15:3,4,12Maana, ikiwa twaamini ya kwamba Yesu alikufa akafufuka, vivyo hivyo na hao waliolala katika Yesu, Mungu atawaleta pamoja naye. 15#1 Kor 15:51-52; 7:10,25Kwa kuwa twawaambieni haya kwa neno la Bwana, kwamba sisi tulio hai, tutakaosalia hata wakati wa kuja kwake Bwana, hakika hatutawatangulia wao waliokwisha kulala mauti. 16#1 Kor 15:52; 2 The 1:7Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza. 17#Yn 12:26; 17:24Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele. 18Basi, farijianeni kwa maneno hayo.
Actualmente seleccionado:
1 The 4: SUV
Destacar
Compartir
Copiar

¿Quieres guardar tus resaltados en todos tus dispositivos? Regístrate o Inicia sesión
Swahili Union Version (SUV): © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 1952, 1997. All rights reserved. lt/pgt ltpgtSwahili Union Version (SUV): Hakimiliki -1952, 1997: kwa: Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.