Zaburi 5
5
Sala wakati wa hatari
(Kwa Mwimbishaji: Na filimbi. Zaburi ya Daudi)
1Usikilize maneno yangu, ee Mwenyezi-Mungu,
usikie ninavyopiga kite.
2Usikilize kilio changu,
Mfalme wangu na Mungu wangu,
maana wewe ndiwe nikuombaye.
3Ee Mwenyezi-Mungu, alfajiri waisikia sauti yangu,
asubuhi nakutolea tambiko#5:3 tambiko: Au sala. yangu,
kisha nangojea unijibu.
4Wewe si Mungu apendaye ubaya;
kwako uovu hauwezi kuwako.
5Wenye majivuno hawastahimili mbele yako;
wewe wawachukia wote watendao maovu.
6Wawaangamiza wote wasemao uongo;
wawachukia wauaji na wadanganyifu.
7Lakini, kwa wingi wa fadhili zako,
mimi nitaingia nyumbani mwako;
nitakuabudu kuelekea hekalu lako takatifu,
nitakusujudia kwa uchaji.
8Uniongoze, ee Mwenyezi-Mungu, katika uadilifu wako,
maana maadui zangu ni wengi;
uiweke njia yako wazi mbele yangu.
9Vinywani mwao hamna ukweli;
mioyoni mwao wamejaa maangamizi,
wasemacho ni udanganyifu wa kifo,
ndimi zao zimejaa hila.
10Uwaadhibu kwa hatia yao ee Mungu;
waanguke kwa njama zao wenyewe;
wafukuze nje kwa sababu ya dhambi zao nyingi,
kwa sababu wamekuasi wewe.
11Lakini wafurahi wote wanaokimbilia usalama kwako,
waimbe kwa shangwe daima.
Uwalinde wanaolipenda jina lako,
wapate kushangilia kwa sababu yako.
12Maana wewe Mwenyezi-Mungu wawabariki waadilifu;
wawakinga kwa fadhili zako kama kwa ngao.
Currently Selected:
Zaburi 5: BHND
Highlight
Share
Copy
Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in
Biblia Habari Njema kwa Watu Wote (Yenye Vitabu vya Deuterokanoni): Tafsiri ya Ushirikiano wa Makanisa (BHN): Hakimiliki -1995, 2001: kwa Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.
Learn more about Biblia Habari Njema