Mwanzo 5
5
Wazao wa Adamu
(1 Sik 1.1-4)
1Hiki ndicho kitabu cha uzao wa Adamu.
Wakati Mungu alipowaumba wanadamu, aliwaumba kwa mufano wake. 2Aliwaumba mwanaume na mwanamuke, kisha akawabariki na kuwapa jina “Wanadamu” siku ileile alipowaumba.
3Adamu alipokuwa na umri wa miaka mia moja na makumi tatu, alipata mutoto aliyefanana naye, na mwenye sura kama yake; akamwita Seti. 4Kisha kuzaa Seti, Adamu akaishi miaka mia nane, na kupata wana wengine na wabinti. 5Adamu alikufa akiwa na umri wa miaka mia tisa na makumi tatu.
6Wakati Seti alipokuwa na umri wa miaka mia moja na mitano, akazaa Enosi. 7Kisha kuzaa Enosi, Seti akaishi miaka mia nane na saba, na kupata wana wengine na wabinti. 8Seti akakufa akiwa na umri wa miaka mia tisa kumi na miwili.
9Wakati Enosi alipokuwa na umri wa miaka makumi tisa, akazaa Kenani. 10Kisha kuzaa Kenani, Enosi akaishi miaka mia nane kumi na mitano, na kupata wana wengine na wabinti. 11Enosi akakufa akiwa na umri wa miaka mia tisa na mitano.
12Wakati Kenani alipokuwa na umri wa miaka makumi saba, akazaa Mahalaleli. 13Kisha kuzaa Mahalaleli, Kenani akaishi miaka mia nane na makumi ine, na kupata wana wengine na wabinti. 14Kenani alikufa akiwa na umri wa miaka mia tisa na kumi.
15Wakati Mahalaleli alipokuwa na umri wa miaka makumi sita na mitano, akazaa Yaredi. 16Kisha kuzaa Yaredi, Mahalaleli akaishi miaka mia nane na makumi tatu, na kupata wana wengine na wabinti. 17Mahalaleli akakufa akiwa na umri wa miaka mia nane makumi tisa na mitano.
18Wakati Yaredi alipokuwa na umri wa miaka mia moja makumi sita na miwili, akazaa Henoki. 19Kisha kuzaa Henoki, Yaredi akaishi miaka mia nane, na kupata wana wengine na wabinti. 20Yaredi akakufa akiwa na umri wa miaka mia tisa makumi sita na miwili.
21Wakati Enoki alipokuwa na umri wa miaka makumi sita na mitano, akazaa Metusela. 22Enoki alikuwa anashirikiana na Mungu. Kisha kuzaa Metusela, Enoki aliishi miaka mia tatu, na kupata wana wengine na wabinti. 23Enoki aliishi miaka mia tatu makumi sita na mitano. 24Alikuwa akishirikiana na Mungu, akatoweka, kwa maana Mungu alimupeleka.
25Wakati Metusela alipokuwa na umri wa miaka mia moja makumi nane na saba, akazaa Lameki. 26Kisha kuzaa Lameki, Metusela akaishi miaka mia saba makumi nane na miwili, na kupata wana wengine na wabinti. 27Metusela akakufa akiwa na umri wa miaka mia tisa makumi sita na tisa.
28Wakati Lameki alipokuwa na umri wa miaka mia moja makumi nane na miwili, akazaa mutoto mwanaume. 29Akamwita mutoto yule Noa, akisema: “Mutoto huyu ndiye atakayetufariji kutokana na kazi yetu ngumu tunayofanya kwa mikono yetu katika inchi ambayo Yawe alilaani.” 30Kisha kuzaa Noa, Lameki akaishi miaka mia tano makumi kenda na mitano, na kupata wana wengine na wabinti. 31Lameki akakufa akiwa na umri wa miaka mia saba makumi saba na saba.
32Kisha Noa kutimiza umri wa miaka mia tano, akazaa Semu na Hamu na Yafeti.
Currently Selected:
Mwanzo 5: SWC02
Highlight
Share
Copy
Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in
Bible in Swahili Congo © Bible Society of the Democratic Republic of Congo (DRC), 2002.