Luka 13
13
Acheni dhambi zenu au mtakufa
1Wakati huo watu fulani walikuja, wakamweleza Yesu juu ya watu wa Galilaya ambao Pilato#13:1 Pilato: Mtawala au gavana wa Yudea (Luka 3:1). Hatuna kumbukumbu nyingine za historia kuhusu tukio hili wala lile la aya ya 4. Labda kutokana na ghasia fulani, jeshi la Pilato liliwaua mahujaji kadhaa waliotoka Galilaya wakati uleule walipokuwa wanatambika wanyama wao wa tambiko. Msemo wa neno kwa neno: Alichanganya damu yao na ya tambiko unatumiwa kimfano kusema kwamba kuuawa kwao kulifanyika wakati walipokuwa wanatambikia. alikuwa amewaua wakati walipokuwa wanachinja wanyama wao wa tambiko. 2Naye Yesu akawaambia, “Mnadhani Wagalilaya hao walikuwa wahalifu kuliko Wagalilaya wengine, ati kwa sababu wameteseka hivyo? 3Nawaambieni hakika sivyo; lakini nanyi, hali kadhalika, msipotubu mtaangamia kama wao. 4Au wale kumi na wanane walioangukiwa na mnara kule Siloamu, wakafa; mnadhani wao walikuwa wakosefu kuliko wengine wote walioishi Yerusalemu? 5Nawaambieni sivyo; lakini nanyi msipotubu, mtaangamia kama wao.”
Mfano wa mtini usiozaa#13:6-9 Mfano huu unapatikana tu katika Luka ambaye hana ule mfano wa kukauka ule mtini katika Mat 21:18-22; Marko 11:12-14,20-25). Hapa yahusu mwenendo usio sawa au usiofaa wa Israeli na viongozi wake. Rejea Isa 5:1-7; Yer 2:21; 8:13.
6Kisha, Yesu akawaambia mfano huu: “Mtu mmoja alikuwa na mtini shambani mwake. Mtu huyu akaenda akitaka kuchuma matunda yake, lakini akaukuta haujazaa hata tunda moja. 7Basi, akamwambia mfanyakazi wake: ‘Angalia! Kwa miaka mitatu nimekuwa nikija kuchuma matunda ya mtini huu, bila kupata chochote. Ukate! Kwa nini uitumie ardhi bure?’ 8Lakini yeye akamjibu: ‘Bwana, tuuache tena mwaka huu; nitauzungushia mtaro na kuutilia mbolea. 9Kama ukizaa matunda mwaka ujao, vema; la sivyo, basi utaweza kuukata.’”
Yesu anamponya mama mmoja siku ya Sabato#13:10-17 Ona jinsi sehemu hii na ile ya Luka 14:1-6 zinavyofanana.
10Yesu alikuwa akifundisha katika sunagogi moja siku ya Sabato. 11Na hapo palikuwa na mwanamke mmoja aliyekuwa mgonjwa kwa miaka kumi na minane kutokana na pepo aliyekuwa amempagaa. Kwa sababu hiyo, mwili wake ulikuwa umepindika vibaya hata asiweze kusimama wima. 12Yesu alipomwona, alimwita, akamwambia, “Mama, umeponywa ugonjwa wako.” 13Akamwekea mikono, na mara mwili wake ukawa wima tena, akawa anamtukuza Mungu. 14Lakini mkuu wa sunagogi alikasirika kwa sababu Yesu alikuwa amemponya huyo mama siku ya Sabato. Hivyo akawaambia wale watu waliokusanyika pale, “Mnazo siku sita za kufanya kazi. Basi, fikeni siku hizo mkaponywe magonjwa yenu; lakini msije siku ya Sabato.”#13:14 Kut 20:9-10; Kumb 5:13-14; taz pia Mat 12:10. Kulingana na mapokeo ya waalimu wa Wayahudi ni matukio yaliyohusu uhai na kifo tu ndiyo yaliyoruhusiwa kushughulikiwa siku ya Sabato.
15Hapo Bwana akamjibu, “Enyi wanafiki! Nani kati yenu hangemfungua ng'ombe wake au punda wake kutoka zizini ampeleke kunywa maji, hata kama siku hiyo ni ya Sabato? 16Sasa, hapa yupo binti wa Abrahamu#13:16 Binti wa Abrahamu: Kama tukifikiria kwamba kutokana na desturi za Wayahudi wanawake hawakupewa haki sawa na wanaume, Yesu kwa kumtaja huyo mama kama binti wa Abrahamu (mzawa wa Abrahamu) anampatia hadhi yake ya kuwa mmoja wa watu wa Mungu na mwenye haki kama wengine. ambaye Shetani alimfanya kilema kwa muda wa miaka kumi na minane. Je, haikuwa vizuri kumfungulia vifungo vyake siku ya Sabato?” 17Alipokwisha sema hayo, wapinzani wake waliona aibu lakini watu wengine wote wakajaa furaha kwa sababu ya mambo yote aliyotenda.
Mfano wa mbegu ndogo ya haradali
(Mat 13:33)
18Yesu akauliza: “Ufalme wa Mungu unafanana na nini? Nitaulinganisha na nini?#13:18 Fundisho tunalopewa katika mifano miwili inayofuata (aya 18-19,20-21) ni kwamba ufalme wa Mungu huanza kwa hali ndogo na hata bila kuweza kuonekana, lakini baadaye unaoneshaonesha nguvu yake kuu na kuonekana. 19Ni kama mbegu ya haradali#13:19 Haradali: Mmea mkubwa ambao wajulikana maarufu kwa vile unaota kutokana ma mbegu ndogo sana. Taz Mat 13:31. Kuhusu picha ya ndege katika matawi tazama Eze 17:23; Dan 4:12,21. aliyotwaa mtu mmoja na kuipanda shambani mwake; ikaota na kuwa mti. Ndege wa angani wakajenga viota vyao katika matawi yake.”
Mfano wa chachu
(Mat 13:31-32; Marko 4:30-32)
20Tena akauliza: “Nitaulinganisha ufalme wa Mungu na nini? 21Ni kama chachu aliyoitwaa mama mmoja na kuichanganya pamoja na unga madebe mawili na nusu kisha unga wote ukaumuka.”
Mlango mwembamba
(Mat 7:13-14,21-23)
22Yesu aliendelea na safari yake kwenda Yerusalemu huku akipitia mijini na vijijini, akihubiri. 23Mtu mmoja akamwuliza, “Je, Mwalimu, watu watakaookoka ni wachache?” 24Yesu akawaambia, “Jitahidini kuingia kwa kupitia mlango mwembamba; maana nawaambieni, wengi watajaribu kuingia lakini hawataweza. 25Wakati utakuja ambapo mwenye nyumba atainuka na kufunga mlango. Nyinyi mtasimama nje na kuanza kubisha mlango mkisema: ‘Bwana, tufungulie mlango.’ Lakini yeye atawajibu: ‘Sijui mmetoka wapi.’ 26Nanyi mtaanza kumwambia: ‘Sisi ndio wale tuliokula na kunywa pamoja nawe; na wewe ulifundisha katika vijiji vyetu.’ 27Lakini yeye atasema: ‘Sijui nyinyi mmetoka wapi; ondokeni mbele yangu, enyi nyote watenda maovu.’#13:27 Ondokeni …enyi nyote watenda maovu: Tazama Zab 6:8. 28Ndipo kutakuwa na kulia na kusaga meno, wakati mtakapowaona Abrahamu, Isaka na Yakobo na manabii wote wapo katika ufalme wa Mungu, lakini nyinyi wenyewe mmetupwa nje!#13:28 Picha tunayopewa hapa kwa maneno Kulia na kusaga meno ni ya uchungu na kukata tamaa (taz Mat 22:13; 25:30). 29Watu watakuja kutoka mashariki na magharibi, kutoka kaskazini na kusini na kukaa kwenye karamu katika ufalme wa Mungu. 30Naam, wale walio wa mwisho watakuwa wa kwanza; na wale walio wa kwanza watakuwa wa mwisho.”#13:30 Wa kwanza watakuwa wa mwisho: Inapokuwa ni jambo la ufalme wa Mungu, matazamio na namna ya watu ya kufikiri ni kinyume kabisa; ufalme wa Mungu unaleta mapinduzi.
Upendo wa Yesu kwa Yerusalemu
(Mat 23:37-39)
31Wakati huohuo, Mafarisayo na watu wengine walimwendea Yesu wakamwambia, “Ondoka hapa uende mahali pengine, kwa maana Herode#13:31 Herode: Aitwaye Antipa; tazama Luka 3:1. Eneo la Galilaya alimotoka Yesu lilikuwa chini ya utawala wa huyo Herode. anataka kukuua.” 32Yesu akawajibu, “Nendeni mkamwambie huyo mbweha#13:32 Mbweha: Pengine hata mbwamwitu au fisi. Kwa Wayahudi Mbweha alikuwa mfano wa ujanja na pia hali duni au mtu asiye wa kuthamini, mdhoofu au asiye wa maana (ling Neh 4:3 na Eze 13:4 ambapo neno mbwamwitu lafaa zaidi). Yamkini hapa katika 13:32 ni neno la kupuuza. hivi: ‘Leo na kesho ninafukuza pepo na kuponya wagonjwa, na siku ya tatu nitakamilisha kazi yangu.’ 33Hata hivyo, kwa leo, kesho na kesho kutwa, ni lazima niendelee na safari yangu, kwa sababu si sawa nabii auawe nje ya Yerusalemu.#13:33 Yesu anagusia juu ya kifo chake ambacho kitatokea karibuni; na kusema kwa dhihaka kwamba haifai nabii kufia nje ya Yerusalemu (aya 34) yaani, naye pia, ni sawa kuufuata mkondo huohuo.
34“Yerusalemu! Ee Yerusalemu!#13:34 Yerusalemu! Ee Yerusalemu: Yesu anasemekana katika Mat 23:37-39 kuyasema maneno haya hekaluni, juma la mwisho kabla ya kuteswa kwake. Unawaua manabii na kuwapiga mawe wale waliotumwa kwako. Mara ngapi nimetaka kuwakusanya watoto wako pamoja kama kuku anavyokusanya vifaranga vyake chini ya mabawa yake, lakini hukutaka. 35Haya! Utaachiwa mwenyewe nyumba#13:35 Yer 22:5 “Nyumba”: - yawezekana hapa inamaanisha hekalu pia. yako. Basi, nawaambieni, hamtaniona mpaka wakati utakapofika mseme:#13:35 Mpaka wakati utakapofika mseme: Baadhi ya hati za mkono zina: mpaka wakati mtakaposema (taz Mat 23:39; Zab 118:26). ‘Abarikiwe huyo ajaye kwa jina la Bwana.’”#13:35 Abarikiwe huyo ajaye kwa jina la Bwana: Maneno kutoka Zab 118:26; yanatumiwa kumkaribisha Yesu na kumshangilia pale anapoingia Yerusalemu (19:37-38).
Valgt i Øjeblikket:
Luka 13: BHNTLK
Markering
Del
Kopiér
Vil du have dine markeringer gemt på tværs af alle dine enheder? Tilmeld dig eller log ind
Copyright The Bible Society of Tanzania, 1993
The Bible Society of Kenya 1993