Luka 12
12
Onyo kuhusu unafiki
1Wakati watu kwa maelfu walipokuwa wamekusanyika hata wakawa wanakanyagana, Yesu aliwaambia kwanza wanafunzi wake, “Jihadharini na chachu#12:1 Chachu: Tazama Mat 13:33. Kama vile chachu hupenya donge la unga wa mkate na kuuchachusha, uongo au unafiki umewapenya na kuwakumba Mafarisayo wengi (Mat 16:6,12; Marko 8:15). ya Mafarisayo, yaani unafiki.#12:1 Hapa panahusu unafiki wa Mafarisayo ambao hautaweza kubaki umefichika. Taz Mat 10:26; Marko 4:22; Luka 8:17. 2Kila kilichofunikwa kitafunuliwa, kila kilichofichika kitafichuliwa. 3Kwa hiyo, kila mliyosema gizani, watu watayasikia katika mwanga, na kila mliyonong'ona faraghani milango imefungwa, yatatangazwa juu ya nyumba.
Anayestahili kuogopwa
(Mat 10:28-31)
4“Nawaambieni nyinyi rafiki zangu: msiwaogope wale wanaoua mwili, wasiweze kufanya kitu kingine zaidi. 5Nitawaonesheni yule ambaye ni lazima kumwogopa: mwogopeni yule ambaye baada ya kuua ana uwezo wa kumtupa mtu katika moto wa Jehanamu. Naam, ninawaambieni, mwogopeni huyo.#12:5 Kadiri ya ufafanuzi wa kawaida hapa, huyo mwenye uwezo huo ni Mungu (ling na Ebr 10:31; Yak 4:12). “Mwogopeni:” yaani Mungu; neno la Kigiriki linachukua hapa pia wazo la heshima au uchaji (kama katika Luka 1:50; 18:2; 23:40). 6Inajulikana kwamba shomoro#12:6 Shomoro: Ndege ambaye alikuwa na thamani kidogo hivyo kwamba sarafu ndogo mbili zilitosha kumnunua. watano huuzwa kwa sarafu ndogo kumi, au sivyo? Lakini mbele ya Mungu hasahauliki hata mmoja. 7Lakini hata nywele za vichwa vyenu zimehesabiwa zote. Msiogope, basi; nyinyi mna thamani kuliko shomoro wengi!
Kumkiri na kumkana Kristo
(Mat 10:32-33; 12:32; 10:19-20)
8“Nawaambieni kweli, kila mtu anayekiri hadharani kwamba yeye ni wangu, Mwana wa Mtu naye atakiri mbele ya malaika wa Mungu kwamba mtu huyo ni wake. 9Lakini, mtu yeyote anayenikana mbele ya watu, naye atakanwa mbele ya malaika wa Mungu.
10“Yeyote anayesema neno la kumpinga Mwana wa Mtu atasamehewa; lakini anayemkufuru Roho Mtakatifu hatasamehewa.#12:10 Mat 12:32; Marko 3:28-29. Juu ya kinachoitwa “dhambi isiyosamehewa”, tazama Marko 3:30 ambapo Yesu anataja juu ya dhambi isiyosamehewa watu walipomsema kwamba alikuwa anatoa pepo kwa uwezo wa mkuu wa pepo.
11“Watakapowapeleka nyinyi mbele ya masunagogi na mbele ya wakuu na watawala, msiwe na wasiwasi juu ya jinsi mtakavyojitetea au jinsi mtakavyosema. 12Kwa maana wakati huo Roho Mtakatifu atawafundisheni kile mnachopaswa kusema.”
Mfano wa tajiri mpumbavu
13 # 12:13-34 Sehemu hii inaunganisha maelekezo kadha wa kadha ya Yesu jinsi ya kukabiliana na mali na utajiri wa ulimwengu huu; yaani msimamo ambao wanafunzi wake wanapaswa kuwa nao kuhusu mali. Mtu mmoja katika ule umati wa watu akamwambia, “Mwalimu, mwambie ndugu yangu tugawane urithi aliotuachia baba.”#12:13 Mara kwa mara, waalimu wa Wayahudi, walikuwa waamuzi katika masuala kama hayo. Ling na Kumb 21:15-17. 14Yesu akamjibu, “Rafiki, ni nani aliyeniweka mimi kuwa mwamuzi au msuluhishi kati yenu?”
15Basi, akawaambia wote, “Jihadharini na kila aina ya tamaa; maana uhai wa mtu hautegemei#12:15 Hautegemei: Au: Hautokani na. wingi wa vitu alivyo navyo.” 16Kisha akawaambia mfano: “Kulikuwa na tajiri mmoja ambaye shamba lake lilizaa mavuno mengi. 17Tajiri huyo akafikiri moyoni mwake: ‘Nitafanyaje nami sina mahali pa kuhifadhia mavuno yangu? 18Nitafanya hivi: nitabomoa ghala zangu na kujenga kubwa zaidi, nami nitahifadhi humo mavuno yangu yote na mali yangu. 19Hapo nitaweza kuiambia roho yangu: sasa unayo akiba ya matumizi kwa miaka na miaka. Ponda mali, kula, kunywa na kufurahi.’#12:19 Kula, kunywa na kufurahi: Msemo wa kawaida ambao wapatikana hata katika maandishi kadhaa ya kale. Ling na Mhub 8:15. 20Lakini Mungu akamwambia: ‘Mpumbavu wewe; leo usiku roho yako itachukuliwa. Na vitu vile vyote ulivyojirundikia vitakuwa vya nani?’” 21Yesu akamaliza kwa kusema, “Ndivyo ilivyo kwa mtu anayejirundikia mali kwa ajili yake mwenyewe, lakini si tajiri mbele ya Mungu.”
Mtumaini Mungu
(Mat 6:25-34)
22Kisha Yesu akawaambia wanafunzi wake, “Kwa sababu hiyo nawaambieni, msiwe na wasiwasi juu ya chakula mnachohitaji ili kuishi, wala juu ya mavazi mnayohitaji kwa ajili ya miili yenu. 23Kwa sababu uzima ni bora kuliko chakula, na mwili ni bora kuliko mavazi. 24Chukueni kwa mfano, kunguru: hawapandi, hawavuni wala hawana ghala yoyote. Hata hivyo, Mungu huwalisha. Nyinyi mna thamani zaidi kuliko ndege! 25Ni nani kati yenu kwa kuwa na wasiwasi sana anaweza kuongeza kidogo urefu wa maisha yake?#12:25 Anaweza kuongeza kidogo urefu wa maisha yake?: Au: “Anaweza kuongeza kimo chake?” 26Basi, kama hamwezi kufanya jambo dogo kama hilo, kwa nini kuwa na wasiwasi juu ya yale mengine? 27Angalieni maua jinsi yanavyomea. Hayafanyi kazi wala hayafumi. Lakini nawaambieni, hata Solomoni mwenyewe na fahari zake zote hakupata kuvikwa vizuri kama ua mojawapo. 28Ikiwa basi, Mungu hulivika hivyo jani la shambani ambalo leo liko na kesho latupwa motoni, je, si atawafanyia nyinyi zaidi? Enyi watu wenye imani haba!
29“Basi, msivurugike akili, mkihangaika juu ya mtakachokula au mtakachokunywa. 30Kwa maana hayo yote yanahangaikiwa na watu wote wasiomjua Mungu. Baba yenu anajua kwamba mnahitaji vitu hivyo. 31Shughulikeni kwanza juu ya ufalme wa Mungu, na hayo mtapewa kwa ziada.
Utajiri mbinguni
(Mat 6:19-21)
32“Msiogope, enyi kundi dogo! Maana Baba yenu amependa kuwapeni ufalme. 33Uzeni mali yenu mkawape maskini hizo fedha. Jifanyieni mifuko isiyochakaa, na kujiwekea hazina mbinguni ambako haitapungua. Huko wezi hawakaribii, wala nondo hawaharibu. 34Pale ilipo hazina yako, ndipo pia utakapokuwa moyo wako.
Watumishi waangalifu
35“Muwe tayari mmejifunga mkanda kiunoni, na taa zenu ziwe zinawaka; 36muwe kama watumishi wanaomngojea bwana wao arudi kutoka harusini, ili wamfungulie mara atakapobisha. 37Heri yao watumishi wale ambao bwana wao atakaporudi atawakuta wanakesha! Nawaambieni hakika, huyo bwana atajifunga mkanda kiunoni, atawaketisha mezani na kuwahudumia.#12:37 Msemo uliotiwa chumvi kidogo hapa - yeye mwenyewe ndiye aliyefanya hivyo kwa wanafunzi wake (ling Yoh 13:1-16). 38Hata kama atarudi usiku wa manane au alfajiri#12:38 Usiku wa manane au alfajiri: Neno kwa neno: Kesha la kwanza au la pili. Wayahudi waligawa muhula wa usiku katika sehemu tatu ambazo waliziita “Kesha” nao Waroma walikuwa na sehemu nne. Kama ni mtindo wa Kiroma unahusika bwana mwenye nyumba angaliweza kuwasili kabla ya saa tisa usiku; kama mtindo unaotumika hapa ni ule wa Wayahudi, huyo bwana mwenye nyumba angefika alfajiri mapema. na kuwakuta wanakesha, heri yao watumishi hao! 39Jueni kwamba, kama mwenye nyumba angejua saa ambayo mwizi atakuja, angekesha, wala hangeiacha nyumba yake ivunjwe. 40Nanyi, kadhalika muwe tayari, maana Mwana wa Mtu atakuja saa msiyoitazamia.”
Mtumishi mwaminifu na asiye mwaminifu
(Mat 24:45-51)
41Petro akamwambia, “Bwana, mfano huo ni kwa ajili yetu tu, au ni kwa ajili ya watu wote?” 42Bwana akajibu, “Ni nani, basi, aliye mtumishi mwaminifu na mwenye busara, ambaye bwana wake atamweka juu ya watumishi wake ili awape chakula wakati ufaao? 43Heri yake mtumishi huyo ikiwa bwana wake atakaporudi atamkuta akifanya hivyo. 44Hakika atampa madaraka juu ya mali yake yote. 45Lakini, kama mtumishi huyo akijisemea moyoni: ‘Bwana wangu amekawia sana kurudi;’ kisha akaanza kuwapiga watumishi wenzake, wa kiume au wa kike, na kula, kunywa na kulewa, 46bwana wake atarudi siku asiyoitazamia na saa asiyoijua; atamwadhibu mtumishi huyo vibaya#12:46 Atamwadhibu …vibaya: Neno kwa neno: Atamkata vipande viwili. Taz Mat 24:51 ambapo maana nyingine inayoweza kutumiwa kufasiri kitendo hicho ni: Atamfukuza). na kumweka fungu moja na wasioamini. 47Mtumishi ambaye anajua matakwa ya bwana wake lakini hajiweki tayari kufanya anavyotakiwa, atapigwa sana. 48Lakini yule afanyaye yanayostahili adhabu bila kujua, atapigwa kidogo. Aliyepewa vingi atadaiwa vingi; aliyepewa vingi zaidi atadaiwa vingi zaidi.
Yesu ni sababu ya utengano na watu
(Mat 10:34-36)
49“Nimekuja kuwasha moto#12:49 Moto: Labda moto wa hukumu (Mat 7:19; Marko 9:48; Luka 3:16-17) ambao hutenganisha wema mbali na wabaya. (Yamkini Luka anamaanisha hapa Roho Mtakatifu na moto siku ya Pentekoste; linganisha Luka 3:16; Mate 2:3). duniani; laiti ungekuwa umewaka tayari! 50Ninao ubatizo#12:50 Ubatizo: Hapa neno hili latumika kwa mfano kutaja mateso na kifo chake Yesu ambacho kama vile ubatizo ambao husababisha maisha mapya kitasababisha wokovu wa watu. Msemo huu wapatikana katika Luka pekee na ni mojawapo ya misemo ya pekee ambayo Luka ametumia kutaja kifo chake Yesu. Msemo mwingine ni ule wa 9:31 ambao unahusiana na kule kutoka kwa Waisraeli nchini Misri. Katika Marko 10:38 ubatizo linatumiwa sambamba na kikombe (ambacho ni mfano wa mateso). ambao inanipasa niupokee; jinsi gani ninavyohangaika mpaka ukamilike! 51Mnadhani nimekuja kuleta amani duniani? Hata kidogo; si amani bali utengano. 52Na tangu sasa, jamaa ya watu watano itagawanyika; watatu dhidi ya wawili, na wawili dhidi ya watatu. 53Baba atakuwa dhidi ya mwanawe, mwana dhidi ya baba yake; mama dhidi ya bintiye, binti dhidi ya mama yake; mamamkwe dhidi ya mke wa mwanawe na huyo dhidi ya mamamkwe wake.”#12:53 Taz Mika 7:6. Kwa kutumia lugha ya Mika 7:6 Yesu anawatahadharisha wafuasi wake kwamba watateswa na watu wa jamaa zao wenyewe ambao hawashiriki imani yao.
Kufahamu majira
(Mat 16:2-3)
54Yesu akayaambia tena makundi ya watu, “Mnapoona mawingu yakitokea upande wa magharibi, mara mwasema: ‘Mvua itanyesha,’ na kweli hunyesha.#12:54-55 Huko Mashariki ya Kati pepo zilivuma kutoka magharibi, yaani baharini Mediteranea na kuleta mvua huko Palestina; hali pepo zilizovuma kutoka kusini zilikuwa kavu na za joto kutoka huko jangwani. Kila mtu alijua hayo lakini watu walishindwaje kujua ishara za Ufalme wa Mungu? Taz pia 13:1-5; Mat 16:2-3. 55Mnapoona upepo wa kusi unavuma, mwasema ‘Kutakuwa na joto,’ na ndivyo inavyokuwa. 56Enyi wanafiki! Mnajua kutabiri hali ya hewa kwa kuangalia hali ya nchi na anga; kwa nini, basi, hamwezi kujua maana ya nyakati hizi?
Patana na adui yako
(Mat 5:25-26)
57“Na kwa nini hamwezi kujiamulia wenyewe jambo jema la kufanya? 58Maana kama mshtaki wako anakupeleka mahakamani, ingekuwa afadhali kwako kupatana naye mkiwa bado njiani, ili asije akakupeleka mbele ya hakimu, naye hakimu akakutoa kwa polisi, nao wakakutia ndani. 59Hakika hutatoka huko, nakuambia, mpaka utakapomaliza kulipa senti ya mwisho.”
Valgt i Øjeblikket:
Luka 12: BHNTLK
Markering
Del
Kopiér
Vil du have dine markeringer gemt på tværs af alle dine enheder? Tilmeld dig eller log ind
Copyright The Bible Society of Tanzania, 1993
The Bible Society of Kenya 1993