YouVersion Logo
Search Icon

Isaya 34

34
Mungu atawaadhibu maadui zake
1Karibieni mkasikilize enyi mataifa,
tegeni sikio enyi watu.
Sikiliza ee dunia na vyote vilivyomo,
ulimwengu na vyote vitokavyo humo!
2Mwenyezi-Mungu ameyakasirikia mataifa yote,
ameghadhabika dhidi ya majeshi yao yote.
Ameyapangia mwisho wao,
ameyatoa yaangamizwe.
3Maiti zao zitatupwa nje;
harufu ya maiti zao itasambaa;
milima itatiririka damu yao.
4 #34:4 Taz Mat 24:29; Marko 13:25; Luka 21:26; Ufu 6:13-14 Jeshi lote la angani litaharibika,
anga zitakunjamana kama karatasi.
Jeshi lake lote litanyauka,
kama majani ya mzabibu yanyaukavyo,
naam, kama tunda la mtini linyaukavyo.
5 #34:5-17 Taz Isa 63:1-6; Yer 49:7-22; Eze 25:12-14; 35:1-15; Amo 1:11-12; Oba Upanga wa Mungu uko tayari juu mbinguni.
Tazama, washuka kuwaadhibu Waedomu,
watu ambao ameamua kuwaangamiza.
6Upanga utalowa damu na kutapakaa mafuta,
kama kwa damu ya kondoo na mbuzi,
na mafuta ya figo za kondoo dume.
Maana Mwenyezi-Mungu atatoa kafara huko Bosra,
kutakuwa na mauaji makubwa nchini Edomu.
7Nyati wataangamia pamoja nao,
ndama kadhalika na mafahali.
Nchi italoweshwa damu,
udongo utarutubika kwa mafuta yao.
8Maana Mwenyezi-Mungu anayo siku ya kisasi;
mwaka wa kulipiza maadui wa Siyoni.
9Vijito vya Edomu vitatiririka lami,
udongo wake utakuwa madini ya kiberiti;
ardhi yake itakuwa lami iwakayo.
10 #34:10 Taz Ufu 14:11; 19:3 Itawaka usiku na mchana bila kuzimika,
moshi wake utafuka juu milele.
Nchi itakuwa jangwa siku zote,
hakuna atakayepitia huko milele.
11Itakuwa makao ya kozi na nungunungu,
bundi na kunguru wataishi humo.
Mwenyezi-Mungu atawaletea ghasia,
na timazi la fujo kwa wakuu wake.
12Nchi itaitwa “Nchi bila Mfalme;”
wakuu wake wote wametoweka.
13Miiba itaota katika ngome zake,
viwavi na michongoma mabomani mwao.
Itakuwa makao ya mbwamwitu, maskani yao mbuni.
14Pakamwitu na fisi watakuwa humo,
majini#34:14 majini: Taz 13:21 na maelezo. yataitana humo;
kwao usiku utakuwa mwanga,
na humo watapata mahali pa kupumzikia.
15Humo bundi watataga mayai na kuyaatamia,
wataangua vifaranga na kuviweka kivulini mwao.
Humo vipanga watakutania,
kila mmoja na mwenzake.
16Someni katika kitabu cha Mwenyezi-Mungu:
“Hakuna hata kiumbe kimoja kitakachokosekana,
kila kimoja kitakuwako na mwenzake.”
Maana Mwenyezi-Mungu mwenyewe ametamka hivyo,
roho yake itawakusanya hao wote.
17Mwenyezi-Mungu amepanga sehemu ya kila mmoja wao,
ametumia kamba kuwapimia nchi hiyo;
wataimiliki milele na milele,
wataishi humo kizazi hata kizazi.

Currently Selected:

Isaya 34: BHN

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy