YouVersion Logo
Search Icon

Wimbo ulio Bora 2

2
1Mimi ni ua la uwandani,#2:1 Uwanda: kwa Kiebrania ni Sharoni.
Ni fahirisi ya mabondeni.
2Kama fahirisi kati ya miiba,
Kadhalika mpenzi wangu kati ya binti.
3 # Mwa 3:6; Ufu 22:1 Kama mpera kati ya miti ya msituni,
Kadhalika mpendwa wangu kati ya vijana.
Niliketi kivulini mwake kwa furaha,
Na matunda yake niliyaonja kuwa matamu.
4Akanileta mpaka nyumba ya karamu,
Na bendera yake juu yangu ni mapenzi.
5Nishibisheni zabibu, niburudisheni kwa mapera,
Kwa maana nimezimia kwa mapenzi.
6 # Wim 8:3 Mkono wake wa kushoto uko chini ya kichwa changu,
Nao wa kulia unanikumbatia!
7Nawasihi, enyi binti za Yerusalemu,
Kwa paa na kwa ayala wa porini,
Msiyachochee mapenzi, wala kuyaamsha,
Hata yatakapoona vema yenyewe.
8 # Yn 10:4 Sikiliza! Ni mpendwa wangu! Tazama, anakuja,
Akiruka milimani, akichachawa vilimani.
9Mpendwa wangu ni kama paa, au ayala.
Tazama, asimama nyuma ya ukuta wetu,
Achungulia dirishani, atazama kimiani.
10Mpendwa wangu alinena, akaniambia,
Ondoka, mpenzi wangu, mzuri wangu, uje zako,
11Maana tazama, majira ya baridi yamepita,
Masika imekwisha, imekwenda zake;
12Maua yatokea katika nchi,
Wakati wa kuimba umefika,
Na sauti ya mwigo husikiwa kwetu.
13Mtini wapevusha tini zake,
Na mizabibu inachanua,
Inatoa harufu yake nzuri;
Ondoka, mpenzi wangu, mzuri wangu, uje zako.
14 # Wim 8:13 Hua wangu, mafichoni mwa jabali,
Katika sitara za, magenge
Nitazame uso wako, nisikie sauti yako,
Maana sauti yako ni tamu na uso wako unapendeza.
15 # Zab 80:13; Eze 13:4; Lk 13:32 Tukamatie mbweha,
Wale mbweha wadogo,
Waiharibuo mizabibu,
Maana mizabibu yetu yachanua.
16 # Wim 6:3 Mpendwa wangu ni wangu, na mimi ni wake;
Hulisha kundi lake penye nyinyoro.
17 # Wim 4:6; Lk 1:78; Rum 13:12; 2 Pet 1:19; Wim 8:14 Hata jua lipunge, na vivuli vikimbie,
Unigeukie, mpendwa wangu,
Nawe uwe kama paa, au ayala,
Juu ya milima ya Betheri.

Currently Selected:

Wimbo ulio Bora 2: SRUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in