YouVersion Logo
Search Icon

Wimbo ulio Bora 3

3
Ndoto za mapenzi
1 # Zab 4:6; 6:6; Isa 26:9 Usiku kitandani nilimtafuta mpendwa wa nafsi yangu,
Nilimtafuta, nisimpate.
2Nikasema, Haya, niondoke nizunguke mjini,
Katika njia zake na viwanjani,
Nimtafute mpendwa wa nafsi yangu.
Nikamtafuta, nisimpate.
3 # Wim 5:7; Isa 21:6-8,11,12 Walinzi wazungukao mjini waliniona;
Je! Mmemwona mpendwa wa nafsi yangu?
4 # Mit 8:17; 4:13; Rum 8:35,39 Kitambo kidogo tu nilipoachana nao,
Nikamwona mpendwa wa nafsi yangu;
Nikamshika, nisimwache tena,
Hata nilipomleta nyumbani mwa mamangu,
Chumbani mwake aliyenizaa.
5 # Wim 2:7 Nawasihi, enyi binti za Yerusalemu,
Kwa paa na kwa ayala wa porini,
Msiyachochee mapenzi, wala kuyaamsha,
Hata yatakapoona vema yenyewe.
Bwana arusi na kundi lake wakaribia
6 # Wim 8:5; Yer 2:2 Ni nani huyu apandaye kutoka nyikani,
Mfano wake ni nguzo za moshi;
Afukizwa manemane na ubani,
Na mavumbi ya manukato yote ya mchuuzi?
7Tazama, ni machela yake Sulemani;
Mashujaa sitini waizunguka,
Wa mashujaa wa Israeli.
8Wote wameshika upanga,
Wamehitimu kupigana;
Kila mtu anao upanga wake pajani
Kwa hofu ya kamsa za usiku.
9Mfalme Sulemani alijitengenezea machela
Ya miti ya Lebanoni;
10 # Mt 22:37; Yn 13:1,34; Rum 5:8; Efe 3:19; 1 Pet 1:7,8 Nguzo zake alizitengeneza za fedha,
Na mgongo wake wa dhahabu,
Kiti chake kimepambwa urujuani,
Gari lake limenakishiwa njumu,
Hiba ya binti za Yerusalemu.
11 # Ufu 11:15; Zab 110:3; Isa 62:5 Tokeni, enyi binti za Sayuni,
Mtazameni Mfalme Sulemani,
Amevaa taji alilovikwa na mamaye,
Siku ya posa yake,
Siku ya furaha ya moyo wake.

Currently Selected:

Wimbo ulio Bora 3: SRUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in