Zaburi 80
80
Sala ya kurejeshwa kwa Israeli
Kwa mwimbishaji: kwa mtindo wa Yungiyungi, Agano. Ya Asafu. Zaburi.
1 #
Kut 25:22; Kum 33:2; 1 Sam 4:4; Zab 89:1 Wewe uchungaye Israeli, usikie,
Wewe umwongozaye Yusufu kama kundi;
Wewe uketiye juu ya makerubi, utoe nuru.
2Mbele ya Efraimu, na Benyamini, na Manase,
Uziamshe nguvu zako,
Uje, utuokoe.
3 #
1 Fal 18:37
Ee Mungu, uturudishe,
Uangaze uso wako nasi tutaokoka.
4Ee BWANA, Mungu wa majeshi, hadi lini
Utayaghadhibikia maombi ya watu wako?
5Umewalisha mkate wa machozi,
Umewanywesha machozi kwa kipimo kikuu.
6Unatufanya sababu ya ugomvi kwa jirani zetu,
Na adui zetu wanacheka wao kwa wao.
7Ee Mungu wa majeshi, uturudishe,
Uangaze uso wako nasi tutaokoka.
8 #
Isa 5:1,7; Yer 2:21; Eze 15:6 Ulileta mzabibu kutoka Misri,
Ukawafukuza mataifa ukaupanda.
9Ulitengeneza nafasi mbele yake,
Nao ukatia mizizi sana ukaijaza nchi.
10Milima ilifunikwa kwa kivuli chake,
Matawi yake ni kama mierezi ya Mungu.
11 #
Kut 23:31; Zab 72:8 Nao uliyaeneza matawi yake hadi baharini,
Na vichipukizi vyake hadi kunako Mto.
12 #
Isa 5:5
Kwa nini umezibomoa kuta zake,
Wakauchuma wote wapitao njiani?
13Nguruwe wa msituni wanauharibu,
Na hayawani wa kondeni wanautafuna.
14 #
Zek 1:12,16,17; Isa 63:15 Ee Mungu wa majeshi, tunakusihi, urudi,
Utazame toka juu uone, uujie mzabibu huu.
15 #
Isa 49:5
Na mche ule ulioupanda
Kwa mkono wako wa kulia;
Na tawi lile ulilolifanya
Kuwa imara kwa nafsi yako.
16Umechomwa moto; umekatwa;
Kwa lawama ya uso wako wanapotea.
17 #
Zab 89:21; Kut 4:22; Zab 110:1; Dan 7:13,14; Yn 5:21-27 Mkono wako na uwe juu yake
Mtu aliye katika mkono wako wa kulia;
Juu ya mwanadamu uliyeimarisha
Kwa nafsi yako;
18Kisha hatutakuacha kwa kurudi nyuma;
Utuhuishe nasi tutaliitia jina lako.
19 #
Hes 6:25; Zab 27:4,9 Ee BWANA, Mungu wa majeshi, uturudishe,
Uangaze uso wako nasi tutaokoka.
Currently Selected:
Zaburi 80: SRUV
Highlight
Share
Copy
Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.