YouVersion Logo
Search Icon

Zaburi 79

79
Ombi la Huruma kwa Yerusalemu
Zaburi ya Asafu
1 # 2 Fal 25:8-10; 2 Nya 36:17-19; Yer 26:18; Yer 52:12-14 Ee Mungu, mataifa wameingia katika urithi wako,
Wamelinajisi hekalu lako takatifu.
Wamefanya Yerusalemu chungu chungu.
2 # Yer 7:33 Wameziacha maiti za watumishi wako
Ziwe chakula cha ndege wa angani.
Na miili ya watauwa wako
Iwe chakula cha wanyama wa nchi.
3 # Ufu 11:9 Wamemwaga damu yao kama maji
Pande zote za Yerusalemu,
Wala hapakuwa na mtu wa kuwazika.
4Tumekuwa lawama kwa jirani zetu,
Mzaha na dhihaka kwao wanaotuzunguka.
5 # Kum 29:20; Eze 36:5 Ee BWANA, hadi lini? Utaona hasira milele?
Wivu wako utawaka kama moto?
6 # Isa 45:4; Zab 53:4 Ukali wako uwamwagie mataifa wasiokujua,
Na falme za hao wasioliitia jina lako.
7Kwa maana wamemla Yakobo,
Na makao yake wameyaharibu.
8 # Isa 43:25 Usikumbuke juu yetu maovu ya baba zetu,
Rehema zako zije kutulaki haraka,
Kwa maana tumeteseka sana.
9 # Yos 7:0; Yer 14:7 Ee Mungu wa wokovu wetu, utusaidie,
Kwa ajili ya utukufu wa jina lako.
Utuokoe, utusamehe dhambi zetu,
Kwa ajili ya jina lako.
10Kwa nini mataifa yaseme,
Yuko wapi Mungu wao?
Kisasi cha damu ya watumishi wako iliyomwagika
Kijulike kati ya mataifa machoni petu.
11 # Hes 14:17 Kuugua kwake aliyefungwa
Na kuingie mbele zako.
Kwa kadiri ya uweza wa mkono wako
Uwahifadhi waliohukumiwa kufa.
12Uwalipe jirani zetu mara saba vifuani mwao
Laumu zao walizokulaumu, Ee Bwana.
13 # Isa 43:21 Na sisi tulio watu wako,
Na kondoo za malisho yako,
Tutakushukuru milele;
Tutazisimulia sifa zako kizazi hadi kizazi.

Currently Selected:

Zaburi 79: SRUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in