YouVersion Logo
Search Icon

Zaburi 33

33
Ukuu na wema wa Mungu
1Mpigieni BWANA vigelegele, enyi wenye haki,
Kusifu kunawapasa wanyofu wa moyo.
2Mshukuruni BWANA kwa kinubi,
Kwa kinanda cha nyuzi kumi mwimbieni sifa.
3 # Isa 42:10 Mwimbieni wimbo mpya,
Pigeni kwa ustadi kwa sauti ya shangwe.
4Kwa kuwa neno la BWANA lina adili,
Na kazi yake yote huitenda kwa uaminifu.
5Huzipenda haki na hukumu,
Nchi imejaa fadhili za BWANA.
6 # Yn 1:1-3; Ebr 11:3; Ayu 26:13 Kwa neno la BWANA mbingu ziliumbwa,
Na jeshi lake lote kwa pumzi ya kinywa chake.
7Hukusanya maji ya bahari chungu chungu,
Huviweka vilindi katika ghala.
8Nchi yote na imwogope BWANA,
Wote wakaao duniani na wamche.
9 # Mwa 1:3 Maana Yeye alisema, na ikawa;
Na Yeye aliamuru, ikaumbika.
10BWANA huyabatilisha mashauri ya mataifa,
Huitangua mipango ya watu.
11 # Ayu 23:13; Mit 19:21; Eze 38:10; Mdo 4:27,28 Shauri la BWANA lasimama milele,
Makusudi ya moyo wake vizazi na vizazi.
12Heri taifa ambalo BWANA ni Mungu wao,
Watu aliowachagua kuwa urithi wake.
13 # 2 Nya 16:9; Ayu 28:24; Zab 11:4 Toka mbinguni BWANA huchungulia,
Huangalia na kuwaona wanadamu wote.
14Akiwa katika kiti chake cha enzi.
Huwaangalia wote wakaao duniani.
15 # Isa 64:8; Ayu 11:11; Zab 44:21; Mit 24:12; Yer 32:19; Hes 7:2 Yeye aiumbaye mioyo yao wote
Na kuziona kazi zao zote.
16Mfalme haokolewi kwa jeshi lake kubwa,
Wala shujaa haokoki kwa kuwa na nguvu nyingi.
17Farasi hafai kitu kwa wokovu,
Wala hamponyi mtu kwa wingi wa nguvu zake.
18 # Ayu 36:7; Zab 34:15 Tazama, jicho la BWANA li kwao wamchao,
Wazingojeao fadhili zake.
19Ili kuwaponya nafsi zao kutoka kwa mauti,
Na kuwahuisha wakati wa njaa.
20Nafsi zetu zinamngoja BWANA;
Yeye ndiye msaada wetu na ngao yetu.
21Maana mioyo yetu itamfurahia,
Kwa kuwa tumelitumainia jina lake takatifu.
22Ee BWANA, fadhili zako zikae nasi,
Kama tunavyo kutumainia Wewe.

Currently Selected:

Zaburi 33: SRUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in