YouVersion Logo
Search Icon

Zaburi 32

32
Shangwe kwa kusamehewa
Ya Daudi. Funzo
1 # Rum 4:7-8; Zab 85:2 Heri aliyesamehewa dhambi,
Na kuondolewa makosa yake.
2 # Law 17:4; Rum 5:13; Yn 1:47; 2 Kor 1:12 Heri ambaye BWANA hamhesabii hatia,
Na ambaye rohoni mwake hamna hila.
3Nilipokosa kuungama dhambi zangu, mifupa yangu ilipooza
Kwa kulia kwangu mchana kutwa.
4Kwa maana mchana na usiku
Mkono wako ulinilemea.
Jasho langu likakauka hata nikawa
Kama nchi kavu wakati wa kaskazi.
5 # Mit 28:13; Isa 65:24; Lk 15:18 Ndipo nikakuungamia dhambi yangu,
Wala sikuuficha upotovu wangu.
Nilisema, Nitayakiri maasi yangu kwa BWANA,
Nawe ukanisamehe upotovu wa dhambi yangu.
6 # 1 Tim 1:16; Isa 55:6; Yn 7:34 Kwa hiyo, hebu kila akuaminiye
Akuombe awapo katika dhiki.
Hakika maji makuu yafurikapo,
Hayatamfikia yeye.
7 # Zab 9:9; Mit 18:10; Isa 4:6; Mt 23:37; Kol 3:3 Kimbilio langu utanilinda nisipate mateso,
Utanizungusha nyimbo za kufurahia wokovu wangu.
8 # Isa 48:17 Nitakufundisha na kukuonesha njia utakayoiendea;
Nitakushauri, jicho langu likikutazama.
9Msiwe kama farasi wala nyumbu,
Wasiokuwa na akili.
Kwa matandiko ya lijamu na hatamu
Sharti kuwazuia hao, au hawatakukaribia.
10 # Mit 13:21; Zab 34:8; Mit 16:20; Yer 17:7 Naye mtu mwovu ana mapigo mengi,
Bali amtumainiaye BWANA fadhili zitamzunguka.
11Mfurahieni BWANA;
Shangilieni, enyi wenye haki
Pigeni vigelegele vya furaha;
Ninyi nyote mlio wanyofu wa moyo.

Currently Selected:

Zaburi 32: SRUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in