YouVersion Logo
Search Icon

Mithali 30

30
KITABU CHA TANO
Maneno ya Aguri yenye hekima
1Maneno ya Aguri mwana wa Yake; mausia mtu huyu aliyomwambia Ithieli, naam, Ithieli na Ukali.
2 # Zab 73:22 Hakika nimekuwa kama mnyama, wala si mtu;
Wala sina ufahamu wa mwanadamu;
3Wala sikujifunza hekima;
Wala sina maarifa ya kumjua Mtakatifu.
4 # Yn 3:13; Ayu 38:4 Ni nani aliyepanda mbinguni na kushuka chini?
Ni nani aliyekamata upepo kwa makonzi yake?
Ni nani aliyeyafunga maji ndani ya nguo yake?
Ni nani aliyefanya imara ncha zote za nchi?
Jina lake ni nani? Na ni nani jina la mwanawe, kama wajua?
5 # Zab 12:6; 18:30; 84:11 Kila neno la Mungu limehakikishwa;
Yeye ni ngao yao wamwaminio.
6 # Kum 4:2; Ufu 22:18 Usiongeze neno katika maneno yake;
Asije akakulaumu, ukaonekana u mwongo.
7Mambo haya mawili nimekuomba;
Usininyime [matatu] kabla sijafa.
8 # Mt 6:11 Uniondolee ubatili na uongo;
Usinipe umaskini wala utajiri;
Unilishe chakula kilicho kadiri yangu.
9 # Kum 8:12; Neh 9:25; Hos 13:6 Nisije nikashiba nikakukana,
Nikasema, BWANA ni nani?
Wala nisiwe maskini sana nikaiba,
Na kulitaja bure jina la Mungu wangu.
10Usimchongee mtumwa kwa bwana wake;
Asije akakulaani, ukaonekana una hatia.
11Kuna kizazi cha watu wamlaanio baba yao;
Wala hawambariki mama yao.
12 # Isa 65:5; Lk 18:11; Tit 1:15,16 Kuna kizazi cha watu walio safi machoni pao wenyewe;
Ambao hawakuoshwa uchafu wao.
13Kuna kizazi cha watu ambao macho yao yameinuka kama nini!
Na kope zao zimeinuka sana.
14 # Ayu 29:17; Zab 14:4; Amo 8:4 Kuna kizazi cha watu ambao meno yao ni panga;
Na vigego vyao ni kama visu.
Ili kuwala maskini waondolewe katika nchi, Na wahitaji katika wanadamu.
15Mruba anao binti wawili,
Waliao, Nipe! Nipe!
Kuna vitu vitatu visivyoshiba kamwe,
Naam, vinne visivyosema, Basi!
16 # Mit 27:20; Hab 2:5 Kuzimu; na tumbo lisilozaa;
Nchi isiyoshiba maji; na moto usiosema, Basi!
17 # Mwa 9:22; Law 20:9 Jicho la mtu amdhihakiye babaye,
Na kudharau kumtii mamaye;
Kunguru wa bondeni wataling'oa,
Na vifaranga vya tai watalila.
18Kuna mambo matatu yaliyo ya ajabu kwangu,
Naam, kuna manne nisiyoyafahamu.
19Mwendo wa tai katika hewa;
Na mwendo wa nyoka juu ya mwamba;
Mwendo wa merikebu katikati ya bahari;
Na mwendo wa mtu pamoja na msichana.
20Hivyo ndivyo mwendo wa mwanamke mzinifu;
Hula, akapangusa kinywa chake,
Akasema, Sikufanya uovu.
21Kwa ajili ya mambo matatu nchi hutetemeka,
Naam, kwa ajili ya manne haiwezi kuvumilia.
22 # Mit 19:10; Mhu 10:7 Mtumwa apatapo kuwa mfalme;
Mpumbavu ashibapo chakula;
23Mwanamke mwenye kuchukiza aolewapo;
Na mjakazi aliye mrithi wa bibi yake.
24Kuna viumbe vinne duniani vilivyo vidogo;
Lakini vina akili nyingi sana.
25 # Mit 6:6 Chungu ni watu wasio na nguvu;
Lakini hujiwekea chakula wakati wa joto.
26 # Law 11:5; Zab 104:18 Kwanga ni watu dhaifu;
Lakini hujifanyia nyumba katika miamba.
27Nzige hawana mfalme;
Lakini huenda wote pamoja vikosi vikosi.
28Mjusi hushika kwa mikono yake;
Lakini yumo majumbani mwa wafalme.
29Kuna watatu wenye mwendo wa kupendeza,
Naam, wanne walio na mwendo mzuri.
30Simba aliye hodari kupita wanyama wote;
Wala hatishwi na mwingine yeyote yule;
31Jogoo anayetamba; na beberu;
Na mfalme asimamaye mbele ya watu wake.#30:31 Katika Kiebrania maana sio dhahiri.
32 # Mhu 8:3; Mik 7:16; Rum 3:19 Ikiwa umefanya kipumbavu kwa kujikuza;
Au ikiwa umewaza mabaya;
Basi weka mkono wako juu ya kinywa chako.
33Kwa maana kupiga maziwa huleta siagi;
Na kupiga pua hutokeza damu;
kadhalika kuchochea hasira hutokeza ugomvi.

Currently Selected:

Mithali 30: SRUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in