YouVersion Logo
Search Icon

Mithali 29

29
1Aonywaye mara nyingi akishupaza shingo,
Atavunjika ghafla, wala hapati dawa.
2Wenye haki wakiwa na amri, watu hufurahi;
Bali mwovu atawalapo, watu huugua.
3 # 1 Fal 1:48; Flp 2:22; Mit 10:1; 15:20 Apendaye hekima humfurahisha babaye;
Bali ashikamanaye na makahaba hutapanya mali.
4Mfalme huithibitisha nchi kwa hukumu;
Bali yeye apokeaye rushwa huipindua.
5Mwenye kujipendekeza kwa jirani yake,
Hutandika wavu ili kuitega miguu yake.
6Kuna mtego katika kosa la mtu mbaya;
Bali mwenye haki huimba na kufurahi.
7 # Ayu 29:16; Zab 31:7; Isa 35:3,4; Lk 22:32; Gal 6:1 Mwenye haki huyaangalia madai ya maskini;
Bali mtu mbaya hana ufahamu hata ayajue.
8Watu wenye dharau huwasha mji moto;
Bali wenye hekima hugeuzia mbali ghadhabu.
9Mwenye hekima akijadiliana na mpumbavu;
Akikasirika au akicheka, pia hapana raha.
10Wamwagao damu humchukia mtu mkamilifu;
Bali wenye haki humtunza nafsi yake.
11Mpumbavu hudhihirisha hasira yake yote;
Bali mwenye hekima huizuia na kuituliza.
12Mwenye kutawala akisikiliza uongo;
Basi watumishi wake wote watakuwa waovu.
13 # Mt 5:45 Maskini na mdhalimu hukutana pamoja;
BWANA huwatia nuru macho yao wote wawili.
14 # Zab 72:2 Mfalme awahukumuye maskini kwa uaminifu;
Kiti chake cha enzi kitathibitika milele.
15Fimbo na maonyo hutia hekima;
Bali mwana aliyeachiliwa humwaibisha mamaye.
16 # Zab 37:36 Waovu wakiongezeka, maasi huongezeka;
Bali wenye haki watayatazama maanguko yao.
17 # Mit 13:24 Mrudi mwanao naye atakustarehesha;
Naam, atakufurahisha nafsi yako.
18 # 1 Sam 3:1; Amo 8:11; Yn 13:17; Yak 1:25 Pasipo maono, watu huacha kujizuia;
Bali ana heri mtu yule aishikaye sheria.
19Haitoshi mtumwa kuonywa kwa maneno;
Maana ajapoyafahamu hataitika.
20Je! Umemwona mtu mwenye kuhamaki katika maneno?
Afadhali kumtumaini mpumbavu kuliko yeye.
21Amwendekezaye mtumwa wake tangu utoto,
Mwisho wake atakuwa ni mwanawe.
22Mtu wa hasira huchochea ugomvi;
Na mtu mwenye ghadhabu huasi sana.
23 # Isa 2:11,12; Mt 23:12; Lk 14:11 Kiburi cha mtu kitamshusha;
Bali mwenye roho ya unyenyekevu ataheshimiwa.
24 # Law 5:1 Mshiriki wa mwizi huichukia nafsi yake mwenyewe;
Asikia maapizo, wala hana neno.
25 # Mwa 12:12 Kuwaogopa wanadamu huleta mtego;
Bali amtumainiye BWANA atakuwa salama.
26Watu wengi hutafuta upendeleo wa mkuu;
Bali hukumu ya kila mtu hutoka kwa BWANA
27Mtu aliye dhalimu ni chukizo kwa wenye haki;
Na mnyofu wa mwenendo ni chukizo kwa waovu.

Currently Selected:

Mithali 29: SRUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy