Ayubu 25
25
Bildadi anena: Mtu awezaje kuwa mwenye haki mbele za Mungu
1Ndipo Bildadi, Mshuhi, akajibu, na kusema,
2Enzi na hofu zi pamoja na Mungu;#25:2 Katika Kiebrania ni naye.
Hufanya amani katika mahali pake palipoinuka.
3 #
Mwa 1:3-5,14-16; Zab 19:4-6; 139:8,11; Mt 5:45; Yak 1:17 Je! Majeshi yake yahesabika?
Ni nani asiyetokewa na mwanga wake?
4 #
Ayu 4:17; 9:2; Zab 130:3; 143:2; Rum 3:19,20 Basi mtu awezaje kuwa na haki mbele ya Mungu?
Au awezaje kuwa safi aliyezaliwa na mwanamke?
5Tazama, hata mwezi hauangazi,
Wala nyota si safi machoni pake;
6 #
Zab 22:6
Seuze mtu, aliye mdudu!
Na mwanadamu, ambaye ni buu!
Currently Selected:
Ayubu 25: SRUV
Highlight
Share
Copy
Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.