YouVersion Logo
Search Icon

Ayubu 25

25
Bildadi anena: Mtu awezaje kuwa mwenye haki mbele za Mungu
1Ndipo Bildadi, Mshuhi, akajibu, na kusema,
2Enzi na hofu zi pamoja na Mungu;#25:2 Katika Kiebrania ni naye.
Hufanya amani katika mahali pake palipoinuka.
3 # Mwa 1:3-5,14-16; Zab 19:4-6; 139:8,11; Mt 5:45; Yak 1:17 Je! Majeshi yake yahesabika?
Ni nani asiyetokewa na mwanga wake?
4 # Ayu 4:17; 9:2; Zab 130:3; 143:2; Rum 3:19,20 Basi mtu awezaje kuwa na haki mbele ya Mungu?
Au awezaje kuwa safi aliyezaliwa na mwanamke?
5Tazama, hata mwezi hauangazi,
Wala nyota si safi machoni pake;
6 # Zab 22:6 Seuze mtu, aliye mdudu!
Na mwanadamu, ambaye ni buu!

Currently Selected:

Ayubu 25: SRUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in