Isaya 7
7
Isaya amhakikishia mfalme Ahazi
1 #
2 Fal 16:5; 2 Nya 28:5-6 Hata ikawa katika siku za Ahazi, mwana wa Yothamu, mwana wa Uzia, mfalme wa Yuda, Resini, mfalme wa Shamu, na Peka, mwana wa Remalia, mfalme wa Israeli, wakapanda wakaenda Yerusalemu ili kupigana nao, lakini hawakuweza kuushinda. 2Kisha watu wa nyumba ya Daudi wakaambiwa kwamba Shamu wamefanya mapatano na Efraimu. Na moyo wake ukataharuki, na moyo wa watu wake, kama miti ya mwituni itikiswavyo na upepo.
3 #
2 Fal 18:17; Isa 36:2 Basi BWANA akamwambia Isaya, Haya, toka, umlaki Ahazi, wewe na Shear-yashubu#7:3 Kwa maana: mabaki watarudi. mwana wako, huko mwisho wa mfereji wa birika la juu, katika njia kuu ya Uwanja wa Dobi; 4ukamwambie, Hadhari, tulia; usiogope wala usife moyo, kwa sababu ya mikia hii miwili ya vinga hivi vitokavyo moshi; kwa sababu ya hasira kali ya Resini na Shamu, na mwana wa Remalia. 5Kwa kuwa Shamu amekusudia mabaya juu yako, pamoja na Efraimu na mwana wa Remalia, wakisema, 6Haya, na tupande ili kupigana na Yuda na kuwasumbua, tukabomoe mahali tupate kuingia, na kummilikisha mfalme ndani yake, huyo mwana wa Tabeeli. 7Bwana MUNGU asema hivi, Neno hili halitasimama wala halitakuwa. 8#2 Sam 8:6 Kwa maana kichwa cha Shamu ni Dameski, na kichwa cha Dameski ni Resini; na katika muda wa miaka sitini na mitano Efraimu atavunjika vipande vipande, asiwe kabila la watu tena; 9tena kichwa cha Efraimu ni Samaria, na kichwa cha Samaria ni mwana wa Remalia. Ikiwa hamtasimama imara katika imani, hamtathibitika kamwe.
Isaya ampa Ahazi ishara ya Imanueli
10Tena BWANA akasema na Ahazi akinena, 11Jitakie ishara ya BWANA, Mungu wako; itake katika mahali palipo chini sana, au katika mahali palipo juu sana. 12Lakini Ahazi akasema, Sitaitaka, wala sitamjaribu BWANA. 13#Mt 1:23; Lk 1:35; Isa 9:6; 1 Tim 3:16 Naye akasema, Sikilizeni sasa, enyi nyumba ya Daudi; Je! Ni neno dogo kwenu kuwachosha wanadamu, hata mkataka kumchosha Mungu wangu pia? 14Kwa hiyo Bwana mwenyewe atawapa ishara. Tazama, bikira atachukua mimba, atazaa mtoto wa kiume, naye atamwita jina lake Imanueli. 15Siagi na asali atakula, wakati ajuapo kuyakataa mabaya na kuyachagua mema. 16#2 Fal 15:30 Kwa maana kabla mtoto huyo hajajua kuyakataa mabaya na kuyachagua mema, nchi ile, ambayo wewe unawachukia wafalme wake wawili, itaachwa ukiwa. 17#2 Nya 28:19; Neh 9:32; Isa 8:7,8; 1 Fal 12:16 BWANA ataleta juu yako, na juu ya watu wako, na juu ya nyumba ya baba yako, siku zisizokuja bado, tangu siku ile aliyoondoka Efraimu kutoka katika Yuda; yaani, mfalme wa Ashuru.
18Tena itakuwa katika siku hiyo BWANA atampigia kelele inzi aliye katika pande za mwisho za mito ya Misri, na nyuki aliye katika nchi ya Ashuru 19Nao watakuja na kutulia katika mabonde yaliyo ukiwa, na katika pango za majabali, na juu ya michongoma yote, na juu ya malisho yote.
20 #
2 Fal 16:7; Isa 10:5,6; Yer 27:6,7 Katika siku hiyo Bwana atanyoa kichwa na malaika ya miguuni, kwa wembe ulioajiriwa pande za ng'ambo ya Mto, yaani, kwa mfalme wa Ashuru, nao utaziondoa ndevu pia.
21Katika siku hiyo itakuwa ya kwamba mtu atalisha ng'ombe jike mchanga na kondoo wawili wa kike; 22kisha itakuwa, kwa sababu wanyama hao watatoa maziwa mengi, atakula siagi; kwa maana kila mtu aliyesalia katika nchi hii atakula siagi na asali.
23Tena itakuwa katika siku hiyo kila mahali palipokuwa na mizabibu elfu moja, iliyopata fedha elfu moja, patakuwa mahali pa mbigili na miiba tu. 24Mtu atakayekwenda huko atakwenda na mishale na upinde; kwa sababu nchi yote itakuwa ina mbigili na miiba. 25Na vilima vyote vilivyolimwa kwa jembe, hutafika huko kwa sababu ya kuiogopa mbigili na miiba, lakini hapo patakuwa mahali pa kupeleka ng'ombe, mahali pa kukanyagwa na kondoo.
Currently Selected:
Isaya 7: SRUV
Highlight
Share
Copy
Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.