YouVersion Logo
Search Icon

Isaya 8

8
Mwana wa Isaya kuwa ishara ya uvamizi wa Ashuru
1BWANA akaniambia, Ujipatie ubao mkubwa ukaandike juu yake kwa hati ya kawaida, Kwa Maher-shalal-hash-bazi;#8:1 Kwa maana ya ‘kuteka kasi, kupokonya upesi’. 2#2 Fal 16:10 nami nitajipatia mashahidi waaminifu ili kuandika habari, yaani, Uria, kuhani, na Zekaria, mwana wa Yeberekia. 3Nami nikalala na nabii mwanamke, naye akapata mimba, akazaa mtoto wa kiume. Kisha BWANA akaniambia, Mwite jina lake Maher-shalal-hash-bazi. 4#Isa 7:16 Kwa maana kabla mtoto huyo hajaweza kujua kusema, Baba yangu, na Mama yangu, hazina za Dameski na mateka ya Samaria yatachukuliwa mbele ya mfalme wa Ashuru.
5Kisha BWANA akasema nami mara ya pili, akaniambia, 6#Neh 3:15; Yn 9:7 Kwa sababu watu hawa wameyakataa maji ya Shiloa yapitayo polepole, na kufurahi kwa ajili ya Resini na huyo mwana wa Remalia, 7basi sasa angalia; Bwana aleta juu yao maji ya huo Mto, yenye nguvu, mengi sana, nayo ni mfalme wa Ashuru na utukufu wake wote; naye atakuja, na kupita juu ya mifereji yake yote, atafurika juu ya kingo zake zote; 8#Isa 7:14; Mt 1:23 naye atapita, atapita kwa kasi na kuingia Yuda; atafurika na kupita katikati, atafika hadi shingoni; na kule kuyanyosha mabawa yake kutaujaza upana wa nchi yako, Ee Imanueli.
9Ungameni pamoja, enyi makabila ya watu,
Nanyi mtavunjwa vipande vipande;
Tegeni masikio, ninyi nyote wa nchi zilizo mbali;
Jitahidini, nanyi mtavunjwa vipande vipande;
Jitahidini, nanyi mtavunjwa vipande vipande.
10 # Ayu 5:12; Kum 20:1; Yos 1:5; Zab 46:7,11; Isa 9:6; Mt 1:23; Rum 8:31 Fanyeni shauri pamoja, nalo litabatilika;
Semeni neno, lakini halitasimama;
Kwa maana Mungu yu pamoja nasi.
11Maana BWANA aliniambia hivi, kwa mkono hodari, akanifundisha nisiende katika njia ya watu hawa, akisema, 12#1 Pet 3:14-15 Msiseme, Ni njama, kuhusu mambo yote ambayo watu hawa watasema, Ni njama; msihofu kwa hofu yao, wala msiogope. 13#Hes 20:12; Lk 12:5 BWANA wa majeshi ndiye mtakayemtakasa; na awe yeye hofu yenu, na awe yeye utisho wenu. 14#Eze 11:16; Lk 2:24; Rum 9:33; 1 Pet 2:8 Naye atakuwa ni mahali patakatifu; bali ni jiwe la kujikwaza na mwamba wa kujikwaa kwa nyumba za Israeli zote mbili, na mtego na tanzi kwa wenyeji wa Yerusalemu. 15#Lk 20:18 Na wengi watajikwaa juu yake, na kuanguka na kuvunjika, na kunaswa na kukamatwa.
Wafuasi wa Isaya
16 # Dan 12:4 Ufunge huo ushuhuda, ukaitie mhuri sheria kati ya wanafunzi wangu. 17#Hab 2:3; Lk 2:25; Ebr 2:13 Nami nitamngojea BWANA, awafichaye uso wake nyumba ya Yakobo, nami nitamtazamia. 18#Zek 3:8; Ebr 2:13 Angalieni, mimi na watoto hawa niliopewa na BWANA tu ishara na ajabu katika Israeli, zitokazo kwa BWANA wa majeshi, yeye akaaye katika mlima Sayuni.
19 # Zab 106:28 Na wakati watakapokuambia, Tafuta habari kwa watu wenye pepo na kwa wachawi; waliao kama ndege na kunong'ona; je! Haiwapasi watu kutafuta habari kwa Mungu wao? Je! Waende kwa watu waliokufa kwa ajili ya watu walio hai? 20Na waende kwa sheria na ushuhuda; ikiwa hawasemi kulingana na neno hili, bila shaka kwa hao hakuna asubuhi. 21Nao watapita katikati yake, wamedhikika sana na kuwa na njaa; na itakuwa watakapoona njaa, watalalamika na kuapa kwa mfalme wao, na kwa Mungu wao, na kuelekeza nyuso zao juu; 22nao wataiangalia nchi, na, tazama, shida na giza; hapatakuwa changamko kwa sababu ya dhiki; nao watafukuzwa na kuingia katika giza kubwa.

Currently Selected:

Isaya 8: SRUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in