YouVersion Logo
Search Icon

Kutoka 3

3
Mungu amtokea Musa
1 # 1 Fal 19:8 Basi huyo Musa alikuwa akilichunga kundi la Yethro mkwewe, kuhani wa Midiani; akaliongoza kundi nyuma ya jangwa, akafika mpaka mlima wa Mungu, hata Horebu. 2#Mdo 7:30-34; Kum 33:16; Isa 63:9 Malaika wa BWANA akamtokea, katika mwali wa moto uliotoka katikati ya kichaka; akatazama, na kumbe! Kile kichaka kiliwaka moto, nacho kichaka hakikuteketea. 3#Zab 111:2 Musa akasema, Nitageuka sasa niende nione kioja hiki, kwa nini kichaka hiki hakiteketei. 4#Kum 33:16 BWANA alipoona ya kuwa ameenda ili atazame, Mungu akamwita kutoka katikati ya kile kichaka, akasema, Musa! Musa! Akaitika, Mimi hapa. 5#Yos 5:15 Naye akasema, Usikaribie hapa; vua viatu vyako miguuni mwako; maana mahali hapo unaposimama ni mahali patakatifu. 6#Mwa 28:13; Mk 12:26; Isa 6:1,5; Ufu 1:17 Tena akasema, Mimi ni Mungu wa baba yako, Mungu wa Abrahamu, Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo. Musa akafunika uso wake; kwa maana aliogopa kumwangalia Mungu. 7#Mwa 18:21 BWANA akasema, Hakika nimeyaona mateso ya watu wangu walioko Misri, nami nimekisikia kilio chao kwa sababu ya wasimamizi wao; maana nayajua maumivu yao; 8#Mwa 11:5; Kut 12:51; Kum 1:25; Hes 13:27 nami nimeshuka ili niwaokoe kutoka kwa mikono ya Wamisri, niwapandishe kutoka nchi ile, hadi nchi njema, kisha pana; nchi itiririkayo maziwa na asali; hata mahali pa Mkanaani, na Mhiti, na Mwamori, na Mperizi, na Mhivi, na Myebusi. 9#Kut 1:11 Basi, tazama, kilio cha wana wa Israeli kimenifikia; tena nimeyaona hayo mateso ambayo Wamisri wanawatesa. 10#Zab 105:26; Mik 6:4 Haya, basi, nitakutuma sasa kwa Farao, ili upate kuwatoa watu wangu, hao wana wa Israeli, katika Misri.
11 # 1 Sam 18:18; 1 Fal 3:7-9; Isa 6:5,8; Yer 1:6 Musa akamwambia Mungu, Mimi ni nani, hata niende kwa Farao, nikawatoe wana wa Israeli watoke Misri? 12#Mwa 31:3; Kum 31:23; Yos 1:5; Isa 43:2; Rum 8:31 Akasema, Bila shaka mimi nitakuwa pamoja nawe; na dalili ya kuwa nimekutuma ndiyo hii; utakapokuwa umekwisha kuwatoa hao watu katika Misri, mtamwabudu Mungu katika mlima huu.
Mungu afunua jina lake takatifu
13 # Kut 6:2-3; Mwa 32:29 Musa akamwambia Mungu, Tazama, nitakapofika kwa wana wa Israeli, na kuwaambia, Mungu wa baba zenu amenituma kwenu; nao wakaniuliza, Jina lake ni nani? Niwaambie nini? 14#Ufu 1:4,8; Kut 6:3; Yn 8:58; Ebr 13:8 Mungu akamwambia Musa, MIMI NIKO AMBAYE NIKO;#3:14 Au, Nitakuwa kama Nitakavyokuwa; au, Ndimi Ndiye. akasema, Ndivyo utakavyowaambia wana wa Israeli; MIMI NIKO#3:14 Au, Nitakuwa; au, Ndimi. amenituma kwenu.
15 # Zab 135:13; Hos 12:5 Tena Mungu akamwambia Musa, Waambie wana wa Israeli maneno haya, BWANA,#3:15 Neno hili BWANA au MUNGU lionekanapo kuandikwa kwa herufi kubwa, laonesha jina takatifu sana la Mwenyezi Mungu. Katika Kiebrania huwa YHWH (latamkwa Yahweh). Katika Lugha ya Kiebrania neno YHWH laasilika kwa kiarifa ‘hayah’ ambalo tafsiri yake ni ‘kuwa’ Mungu wa baba zenu, Mungu wa Abrahamu, Mungu wa Isaka, Mungu wa Yakobo, amenituma kwenu; hili ndilo jina langu hata milele, nalo ni kumbukumbu langu hata vizazi vyote. 16#Mwa 48:15; 50:24; Kut 2:25; 4:31; Kum 26:7; Zab 80:14; Lk 1:68 Nenda, ukawakusanye wazee wa Israeli pamoja, ukawaambie, BWANA, Mungu wa baba zenu, Mungu wa Abrahamu, Mungu wa Isaka, Mungu wa Yakobo, amenitokea, akaniambia, Hakika nimewajilieni, tena nimeyaona mnayotendewa huko Misri; 17#Mwa 15:14 Nami nimesema, Nitawapandisha kutoka katika mateso ya Misri na kuwaingiza katika nchi ya Mkanaani, na Mhiti, na Mwamori, na Mperizi, na Mhivi, na Myebusi, nchi ijaayo maziwa na asali. 18#Hes 23:3 Nao watakusikia sauti yako; nawe utakwenda, wewe na wazee wa Israeli kwa mfalme wa Misri, na kumwambia, BWANA Mungu wa Waebrania, amekutana nasi; basi sasa twakuomba, tupe ruhusa twende mwendo wa siku tatu jangwani, ili tumtolee dhabihu BWANA Mungu wetu.
19Nami najua ya kuwa huyo mfalme wa Misri hatawapa ruhusa mwende zenu, la, hata kwa mkono wa nguvu. 20#Kut 7:3; 12:31; Kum 6:22; Neh 9:10; Zab 105:27; 135:9; Yer 32:20; Mdo 7:36 Nami nitaunyosha mkono wangu, na kuipiga Misri kwa ajabu zangu zote, nitakazofanya kati yake, kisha baadaye atawapa ruhusa kwenda. 21#Kut 11:3; 12:35-36; Zab 106:46; Mit 16:7 Nami nitawapa watu hao kufadhiliwa mbele ya Wamisri; hata itakuwa, hapo mtakapokwenda zenu hamtakwenda kitupu; 22#Mwa 15:14; Kut 11:2; Ayu 27:17; Mit 13:22; Eze 39:10 Lakini kila mwanamke ataomba kwa jirani, na kwa huyo akaaye naye nyumbani, vyombo vya fedha, na vyombo vya dhahabu, na mavazi; nanyi mtawavika wana wenu na binti zenu; nanyi mtawateka nyara Wamisri.

Currently Selected:

Kutoka 3: SRUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in