Kutoka 2
2
Kuzaliwa na ujana wa Musa
1 #
Kut 6:20; Hes 26:59; 1 Nya 23:13,14 Mtu mmoja wa nyumba ya Lawi akaenda akaoa binti mmoja wa Lawi. 2#Mdo 7:20; Ebr 11:23 Yule mwanamke akachukua mimba akazaa mwana, na alipoona ya kuwa ni mtoto mzuri akamficha miezi mitatu. 3Na alipokuwa hawezi kumficha tena, akamtengenezea kikapu cha mafunjo akakitaliza kwa sifa na lami, akamtia mtoto ndani yake, akakiweka kwenye nyasi kando ya mto. 4#Kut 15:20; Hes 26:59 Dada yake mtoto akasimama mbali ili ajue yatakayompata. 5#Mdo 7:21 Basi binti Farao akashuka, aoge mtoni, na vijakazi wake wakatembea kando ya mto; naye akakiona kile kikapu katika nyasi, akamtuma kijakazi wake kwenda kukileta. 6Akakifungua, akamwona mtoto, na tazama, mtoto yule analia. Basi akamhurumia, akasema, Huyu ni mmojawapo wa watoto wa Waebrania. 7Basi dada yake mtoto akamwambia binti Farao, Je! Niende nikamwite mlezi katika wanawake wa Kiebrania, aje kwako, akunyonyeshee mtoto huyu? 8Binti Farao akamwambia, Haya! Nenda. Yule kijana akaenda akamwita mama yake yule mtoto. 9Binti Farao akamwambia, Mchukue mtoto huyu, ukaninyonyeshee, nami nitakupa mshahara wako. Yule mwanamke akamtwaa mtoto, akamnyonyesha. 10#Mdo 7:21 Mtoto akakua, naye akamleta kwa binti Farao, akawa mwanawe. Akamwita jina lake Musa.#2:10 Jina hili Musa katika Kiebrania ni ‘Mosheh’. Linatokana na neno ‘mashah’ kwa maana ya ‘kutoa’. Katika lugha ya Kimisri neno Musa ni ‘kupata mtoto’, akasema, Kwa sababu nilimtoa majini.
Musa akimbilia Midiani
11 #
Ebr 11:24
Hata siku zile, Musa alipokuwa mtu mzima, akatoka kuwaendea ndugu zake, akatazama mizigo yao. Akamwona Mmisri anampiga Mwebrania, mmojawapo wa ndugu zake.#Mdo 7:23-28 12Basi akatazama huku na huko, na alipoona ya kuwa hapakuwapo mtu, akampiga na kumwua Mmisri yule, akamfukia mchangani. 13Akatoka siku ya pili, na tazama, watu wawili wa Waebrania walikuwa wakipigana. Akamwambia yule aliyemdhulumu mwenzake, Mbona unampiga mwenzako? 14Yule akasema, Ni nani aliyekuweka wewe kuwa mkuu wetu, na mwamuzi juu yetu? Je! Wataka kuniua kama ulivyomwua yule Mmisri? Musa akaogopa, akasema, Kumbe! Jambo lile limejulikana. 15#Mdo 7:29; Ebr 11:27; Mwa 24:11; 29:2 Basi Farao alipopata habari, akataka kumwua Musa; lakini Musa akakimbia kutoka kwa Farao, akakaa katika nchi ya Midiani; akaketi karibu na kisima. 16#Kut 3:1; Mwa 29:10; 1 Sam 9:11 Basi kuhani wa Midiani alikuwa na binti saba, nao wakaja wakateka maji, wakazijaza birika maji, wapate kunywesha kundi la baba yao. 17Wachungaji wakaja wakawafukuza; lakini Musa akasimama, akawasaidia, akalinywesha kundi lao. 18#Hes 10:29 Walipofika kwa Reueli#2:18 Reueli kwa jina jingine aliitwa Yethro, kuhani wa Midiani baba yake Sipora, mkewe Musa. Reueli kwa Kiebrania ni ‘rafiki wa Mungu’ (Kut 2:21; 3:1; 4:18; 18:1-27). baba yao, akasema, Imekuwaje hata mkarejea mapema leo? 19Wakasema, Mmisri mmoja alituokoa katika mikono ya wachungaji, tena zaidi ya hayo, akatutekea maji, akalinywesha kundi. 20#Mwa 31:54 Akawaambia binti zake, Yuko wapi basi? Mbona mmemwacha mtu huyo? Mwiteni, ale chakula. 21Musa akawa radhi kukaa kwake mtu yule, naye akampa Musa binti yake, Sipora. 22#Kut 18:3; Ebr 11:13 Huyo akamzalia mtoto wa kiume, akamwita jina lake Gershomu, maana alisema, Nimekuwa mgeni katika nchi ya ugeni.
23 #
Kut 7:7; Zab 12:5; Mwa 18:20; Kum 24:15; Yak 5:4 Na kisha baada ya muda, yule mfalme wa Misri akafa; wana wa Israeli wakaugua kwa sababu ya ule utumwa, wakalia; kilio chao kikafika juu kwa Mungu kwa sababu ya ule utumwa. 24#Mwa 15:13-14; Kut 6:5; Zab 105:8 Mungu akasikia kuugua kwao, Mungu akakumbuka agano lake alilolifanya na Abrahamu na Isaka na Yakobo. 25#2 Sam 16:12; Lk 1:25 Mungu akawaona wana wa Israeli, na Mungu akawaangalia.
Currently Selected:
Kutoka 2: SRUV
Highlight
Share
Copy
Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.