Kumbukumbu la Torati 18
18
Haki za makuhani na Walawi
1 #
Hes 18:8,9; 1 Kor 9:13 Makuhani Walawi, kabila yote ya Lawi, wasiwe na fungu wala urithi pamoja na Israeli; watakula sadaka za BWANA zifanywazo kwa moto, na urithi wake. 2#Hes 18:20 Wala wasiwe na urithi kati ya ndugu zao; BWANA ndiye urithi wao, kama alivyowaambia. 3#Law 7:30 Na hii itakuwa haki ya makuhani kwa watu hao wasongezao sadaka, ikiwa ni ng'ombe au kondoo wampe kuhani mkono, na mashavu mawili, na tumbo. 4#Kut 22:29; Hes 18:12 Malimbuko ya nafaka zako, na divai yako, na mafuta yako, na manyoya ya kwanza ya kondoo wako, umpe. 5#Kum 10:8 Kwani BWANA, Mungu wako, amemchagua katika kabila zako zote, asimame atumike kwa jina la BWANA, yeye na wanawe milele.
6 #
Hes 35:2,3 Na akija Mlawi atokaye katika malango yako mojawapo, katika Israeli yote alipokuwa akikaa, akaja kwa mapenzi yote ya nafsi yake mahali atakapochagua BWANA; 7na atumike kwa jina la BWANA, Mungu wake, kama wafanyavyo ndugu zake wote, Walawi wasimamao huko mbele za BWANA. 8#2 Nya 31:4; Neh 12:44 Wawe na fungu sawasawa la kula, pamoja na haya yaliyomfikia kwa kuuzwa urithi wa baba zake.
Utoaji watoto kafara, upigaji ramli na uchawi zakatazwa
9 #
Law 18:26; Kum 12:29 Utakapokwisha kuingia katika nchi akupayo BWANA, Mungu wako usijifunze kutenda kwa mfano wa machukizo ya mataifa yale. 10#Law 19:26; Kut 22:18 Asionekane kwako mtu ampitishaye mwanawe au binti yake kati ya moto, wala asionekane mtu atazamaye bao, wala mtu atazamaye nyakati mbaya, wala mwenye kubashiri, wala msihiri, 11#Law 19:31 wala mtu alogaye kwa kupiga mafundo, wala mtu apandishaye pepo, wala mchawi, wala mtu awaombaye wafu. 12#Law 18:24 Kwa maana mtu atendaye hayo ni chukizo kwa BWANA; kisha ni kwa sababu ya hayo BWANA, Mungu wako, anawafukuza mbele yako. 13#Mt 5:48; Mwa 17:1 Uwe mkamilifu kwa BWANA, Mungu wako. 14#2 Fal 21:6 Maana mataifa haya utakaowamiliki huwasikiliza wanaoshika nyakati mbaya na kutazama bao; bali wewe, BWANA, Mungu wako, hakukupa ruhusa kutenda hayo.
Ahadi ya kupewa nabii mpya kama Musa
15 #
Mdo 3:22; 7:37; Hes 24:17; Isa 11:1; 61:1; Mt 11:3; 21:11; Lk 2:25-34; 4:16-22; Lk 7:16; 24:19; Yn 4:19-26; 6:14; 7:40 BWANA, Mungu wako, atakupa nabii miongoni mwa ndugu zako kama nilivyo mimi; msikilizeni yeye. 16Kama vile ulivyotaka kwa BWANA, Mungu wako, huko Horebu, siku ya kusanyiko, ukisema, Nisisikie tena sauti ya BWANA, Mungu wangu, wala nisiuone tena moto huu mkubwa, nisije nikafa. 17BWANA akaniambia, Wametenda vema kusema walivyosema. 18#Yn 1:45; Isa 51:16; Yn 17:8; 4:25; 8:28; 12:49,50 Mimi niwaiwanulia nabii miongoni mwa ndugu zao mfano wako wewe, nami nitatia maneno yangu kinywani mwake, naye atawaambia yote nitakayomwamuru. 19#Mdo 3:23 Hata itakuwa, mtu asiyesikiliza maneno yangu atakayosema yule kwa jina langu, nitalitaka kwake. 20#Kum 13:5; Yer 14:14; Zek 13:3; Yer 2:8 Lakini nabii atakayenena neno kwa kujikinai kwa jina langu, ambalo sikumwagiza kulinena, au atakayenena katika jina la miungu mingine, nabii yule atakufa. 21Nawe ukisema moyoni mwako, Tutajuaje neno asilolinena BWANA? 22#Yer 28:9 Atakaponena nabii kwa jina la BWANA, lisifuate jambo lile wala kutimia, hilo ndilo neno asilolinena BWANA; kwa kujikinai amelinena huyo nabii, usimwogope.
Currently Selected:
Kumbukumbu la Torati 18: SRUV
Highlight
Share
Copy
Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.