YouVersion Logo
Search Icon

Kumbukumbu la Torati 17

17
1Usimchinjie BWANA, Mungu wako, ng'ombe wala kondoo aliye na kilema, wala neno ovu lolote; kwa kuwa hayo ni machukizo kwa BWANA, Mungu wako.
2Ikiwa ameonekana katikati yako, ndani ya malango yako mojawapo, upewayo na BWANA, Mungu wako, mtu mume au mke afanyaye yaliyo maovu machoni pa BWANA, Mungu wako, kwa kuvunja maagano yake, 3#Kut 22:20; Ayu 31:26; Yer 7:22 naye amekwenda kutumikia miungu mingine na kuiabudu, au jua, au mwezi, au vilivyo katika jeshi la mbinguni vyovyote, nisivyoagiza mimi; 4ukiambiwa hayo nawe umeyasikia, ndipo utafute kwa bidii, na tazama, ikiwa ni kweli lina hakika jambo lile, kuwa yafanywa machukizo kama hayo katika Israeli; 5#Law 24:14; Yos 7:25 ndipo umchukue nje malangoni kwako, yule mtu mume, au yule mwanamke, aliyefanya jambo lile ovu; ukawapige kwa mawe, wafe. 6#Hes 35:30; Kum 19:15; Mt 18:16; 2 Kor 13:1; 1 Tim 5:19; Yn 8:17 Huyo atakayeuawa na auawe kwa midomo ya mashahidi wawili, au mashahidi watatu; asiuawe kwa mdomo wa shahidi mmoja. Ebr 10:28 7#1 Kor 5:13 Mikono ya wale mashahidi na iwe juu yake kwanza kwa kumwua, kisha mikono ya watu wote. Uondoe vivyo hivyo uovu katikati yako.
Maamuzi ya makuhani na waamuzi
8 # 2 Nya 19:10; Hag 2:11; Mal 2:7; Kut 21:13; Hes 35:11; Kum 12:5; 19:17; Zab 122:5 Ikiwa limezuka neno lililo zito kukupita wewe, katika maamuzi kati ya damu na damu, na kati ya kesi na kesi, na kati ya pigo na pigo, nayo yashindaniwa katika malango yako; ndipo nawe uondoke, ukwee uende mahali atakapochagua BWANA, Mungu wako; 9#Yer 18:18; Kum 19:17; Amu 4:5; 1 Fal 3:16; Eze 44:24 uwaendee makuhani Walawi, na mwamuzi atakayekuwako siku hizo; uwaulize; nao watakuonesha hukumu ya maamuzi; 10nawe fanya sawasawa na hukumu watakayokuonesha mahali hapo atakapochagua BWANA; nawe tunza kufanya kwa mfano wa yote watakayokufunza; 11kwa mfano wa sheria watakayokufunza, na kwa mfano wa hukumu watakayokuambia, fanya vivyo hivyo; usigeuke katika hukumu watakayokuonesha, kwenda mkono wa kulia wala wa kushoto. 12#Hes 15:30; Ezr 10:8; Hos 4:4; Kum 18:5 Na mtu afanyaye kwa kujikinai, kwa kutomsikiza kuhani asimamaye hapo kwa kumtumikia BWANA, Mungu wako, au mwamuzi, na afe mtu huyo; nawe utauondoa uovu katika Israeli. 13Na hao watu wote watasikia na kuogopa, wasifanye tena kwa kujikinai.
Mipaka ya uwezo wa kifalme
14 # 1 Sam 8:5; 10:19; Hos 13:9 Utakapokwisha kuingia katika nchi akupayo BWANA, Mungu wako ukaimiliki, na kukaa humo; nawe utakaposema, Nitaweka mfalme juu yangu mfano wa mataifa yote yaliyo kandokando yangu; 15#Yer 30:21 usiache kumweka yule atakayechaguliwa na BWANA, Mungu wako, awe mfalme juu yako; umweke mmoja katika ndugu zako awe mfalme juu yako; usimtawaze mgeni juu yako, ambaye si ndugu yako. 16#1 Fal 4:26; 10:28; 2 Nya 1:16; 9:28; Zab 20:7; Isa 31:1; Kut 13:17; Hes 14:3,4; Hos 11:5 Ila asifanye farasi wake kuwa wengi, wala asiwarudishe watu Misri, ili apate kufanya farasi kuwa wengi; kwa kuwa BWANA amewaambia, Tangu sasa msirudie tena njia ile. 17#1 Fal 10:14-22,27; 11:1-8; 2 Nya 1:15; 9:27 Wala asijizidishie wake, ili moyo wake usikengeuke; wala asifanye fedha zake na dhahabu kuwa nyingi mno. 18#2 Fal 11:12; Kum 31:9; 2 Fal 22:8 Tena na iwe, zamani aketipo juu ya kiti cha ufalme wake, ajiandikie nakala ya torati hii katika kitabu, kufuata hicho kilicho mbele ya makuhani Walawi; 19#Yos 1:8; Zab 119:97 na awe nayo, asome humo siku zote atakazoishi; ili apate kujifunza kumcha BWANA, Mungu wake, ayashike maneno yote ya torati hii na amri hizi, kwa kuyafanya; 20#Kum 5:32; 1 Fal 15:5 moyo wake usije ukainuliwa juu ya ndugu zake, wala asikengeuke katika maagizo, kwa mkono wa kulia wala wa kushoto; ili apate kuzifanya siku zake kuwa nyingi katika ufalme wake, yeye na wanawe, katikati ya Israeli.

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in