YouVersion Logo
Search Icon

Kumbukumbu la Torati 16

16
Kuitafakari sikukuu ya Pasaka
1 # Kut 12:1-20; Law 23:5-8; Hes 28:16-25; Yn 18:28; 1 Kor 5:7,8; Ebr 11:28 Utunze mwezi wa Abibu, ukamfanyie Pasaka BWANA, Mungu wako, kwa kuwa ilikuwa ni mwezi wa Abibu alipokutoa Misri usiku BWANA; Mungu wako. 2#Kut 12:5-7; Hes 28:19; 2 Nya 35:7; Mt 26:2; Mk 14:12; Lk 22:8,15; 1 Kor 5:7 Nawe umchinjie Pasaka BWANA, Mungu wako, katika kundi la kondoo na la ng'ombe, mahali atakapochagua BWANA apakalishe jina lake. 3#Kut 12:15,19,39; 13:3; 34:18 Usimle pamoja na mikate iliyotiwa chachu; siku saba utakula naye mikate isiyotiwa chachu, nayo ni mikate ya mateso; kwa maana ulitoka nchi ya Misri kwa haraka; ili upate kukumbuka siku uliyotoka nchi ya Misri, siku zote za maisha yako. 4#Kut 12:10; 34:25 Wala isionekane kwako chachu muda wa siku saba katika mipaka yako yote; wala katika hiyo nyama uchinjayo siku ya kwanza jioni, kisilale chochote usiku kucha hata asubuhi. 5Usimchinje Pasaka ndani ya malango yako yote akupayo BWANA, Mungu wako; 6#Mt 27:46 ila mahali atakapochagua BWANA, Mungu wako, apakalishe jina lake, ndipo mtakapomchinja Pasaka jioni, katika machweo ya jua, kwa wakati kama uliotoka Misri. 7#Kut 12:8; 2 Nya 35:13; 2 Fal 23:23; Yn 2:13; 11:55 Nawe umwoke na kumla mahali atakapochagua BWANA, Mungu wako; kisha asubuhi yake ugeuke uende hemani mwako. 8#Kut 12:16; 13:6; Law 23:8 Siku sita utakula mikate isiyotiwa chachu; na siku ya saba na uwe mkutano mtukufu kwa BWANA, Mungu wako, usifanye kazi yoyote.
Sikukuu ya majuma
9 # Law 23:15-21; Hes 28:26-31; Kut 23:16; 34:22; Mdo 2:1 Jihesabie majuma saba; tangu wakati uanzao kutia mundu katika mmea utaanza kuhesabu majuma saba. 10#Mit 10:22; Yoe 2:14; 1 Kor 16:2 Nawe sikukuu ya majuma umfanyie BWANA, Mungu wako, kwa kutoa sadaka ya hiari ya mkono wako, utakayotoa kwa kadiri akubarikiavyo BWANA, Mungu wako; 11#Lk 14:12 nawe utafurahi mbele ya BWANA, Mungu wako, wewe na mwana wako na binti yako, na mtumwa wako na mjakazi wako, na Mlawi aliye ndani ya malango yako, na mgeni, na yatima, na mjane aliyefiliwa na mumewe, walio katikati yako, katika mahali atakapochagua BWANA, Mungu wako, apakalishe jina lake. 12#Mwa 15:13; Kut 1:11,14; Kum 15:15; 25:6; Zab 105:23,25 Nawe kumbuka kwamba ulikuwa mtumwa huko Misri; tena zishike amri hizi kwa kuzifanya.
Kuitafakari sikukuu ya vibanda
13 # Law 23:33-36,39-43; Hes 29:12-38; Kut 23:16 Fanya sikukuu ya vibanda siku saba, utakapokwisha kuyakusanya yatokayo katika sakafu yako ya nafaka, na katika kinu chako cha divai; 14#Kum 26:11; Neh 8:9; Mhu 9:7; Isa 12:1-6; 25:6-8 nawe utafurahi katika sikukuu yako, wewe, na mwanao, na binti yako, na mtumwa wako, na mjakazi wako, na Mlawi, na mgeni, na yatima, na mjane aliyefiliwa na mumewe, walio ndani ya malango yako. 15Siku saba mfanyie sikukuu BWANA, Mungu wako, mahali atakapochagua BWANA; kwa kuwa BWANA, Mungu wako, atakubariki katika mavuno yako yote, na katika kazi zote za mikono yako, nawe uwe katika kufurahi kabisa. 16Mara tatu kwa mwaka na watokee wana wa kiume wako wote mbele za BWANA, Mungu wako, mahali atakapochagua; katika sikukuu ya mikate isiyotiwa chachu, na katika sikukuu ya majuma, na katika sikukuu ya vibanda; wala wasitokee mbele za BWANA mikono mitupu. 17#2 Kor 8:12 Kila mtu na atoe kama awezavyo, kwa kadiri ya baraka ya BWANA, Mungu wako, alivyokupa.
Waamuzi na wakuu
18Weka waamuzi na maofisa katika malango yako yote akupayo BWANA, Mungu wako, kwa hesabu ya kabila zako; nao wawaamue watu kwa maamuzi ya haki. 19#Kut 23:6-8; Law 19:15; 1 Sam 8:3; 12:3; Ayu 31:21,22; Mit 17:23; 24:23; Mhu 7:7; Isa 1:17,23; Mdo 10:34 Usipotoe maamuzi; wala usipendelee uso wa mtu; wala usitwae rushwa; kwa kuwa rushwa hupofusha macho ya wenye akili, na kugeuza kesi wa wenye haki. 20#Kum 4:1 Yaliyo haki kabisa ndiyo utakayoyafuata, ili upate kuishi na kuirithi nchi upewayo na BWANA, Mungu wako.
Aina ya ibada zilizokatazwa
21 # Kut 34:13; Amu 3:7; 1 Fal 14:15; 16:33; 2 Fal 17:16; 21:3; 2 Nya 33:3 Usipande mti uwao wote kuwa Ashera kwako kando ya madhabahu utakayofanya ya BWANA, Mungu wako. 22#Law 26:1 Wala usisimamishe nguzo; ambayo BWANA, Mungu wako, aichukia.

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy