YouVersion Logo
Search Icon

1 Wafalme 5

5
Maandalizi ya vifaa vya kujengea hekalu
1 # 2 Sam 5:11; Amo 1:9 Ndipo Hiramu, mfalme wa Tiro, akawatuma watumishi wake kwa Sulemani; kwani alikuwa amesikia ya kwamba wamemtia mafuta awe mfalme mahali pa baba yake. Kwa maana Hiramu alikuwa akimpenda Daudi siku zote. 2#2 Nya 2:3 Basi Sulemani akatuma watu kwa Hiramu, akasema, 3#2 Sam 7:5; 1 Nya 22:8; 28:3; 2 Nya 6:6-8 Wajua kuwa Daudi baba yangu hakuweza kujenga nyumba kwa jina la BWANA, Mungu wake, kwa sababu ya vita vilivyomzunguka pande zote, hata BWANA alipowatia watu chini ya nyayo zake. 4#1 Nya 22:9; Zab 72:7; Isa 9:7 Ila leo BWANA, Mungu wangu, amenipa amani kila upande; hakuna adui, wala tukio baya. 5#2 Nya 2:4; 2 Sam 7:12,13; 1 Nya 22:10 Nami, tazama, nakusudia kujenga nyumba kwa jina la BWANA, Mungu wangu, kama BWANA alivyomwambia Daudi baba yangu, akisema, Mwana wako, nitakayemweka katika kiti chake cha enzi mahali pako, ndiye atakayeijenga nyumba kwa jina langu. 6#1 Fal 6:9,10,16,20; 2 Nya 2:8; Eze 27:5 Basi uamuru wanikatie mierezi ya Lebanoni; na watumishi wangu watafuatana na watumishi wako; na ujira wa watumishi wako nitakupa kama utakavyosema; kwa kuwa wajua ya kwamba hakuna kwetu mtu ajuaye kukata miti kama Wasidoni. 7Ikawa, Hiramu aliposikia maneno yake Sulemani, alifurahi sana, akasema, Na ahimidiwe BWANA leo, aliyempa Daudi mwana mwenye akili juu ya watu hawa walio wengi. 8Hiramu akatuma watu kwa Sulemani, akasema, Nimeusikia ujumbe ulionitumia; nami nitafanya kila ulitakalo kuhusu miti ya mierezi, na miti ya miberoshi. 9#1 Fal 9:20,21; 2 Nya 2:16; Ezr 3:7; Eze 27:17; Mdo 12:20 Watumishi wangu wataishusha toka Lebanoni mpaka baharini; nami nitaiendesha baharini, ikifungwa pamoja, mpaka mahali utakaponiagiza, huko nitaifungua ili wewe uichukue; ndivyo utakavyoitimiza haja yangu, ukiwapa chakula watu wa nyumbani mwangu. 10Basi Hiramu akampa Sulemani miti ya mierezi na miti ya miberoshi kadiri alivyotaka. 11#2 Nya 2:10 Sulemani akampa Hiramu kori#5:11 tazama 4:22. elfu ishirini za ngano, chakula cha watu wake, na kori ishirini za mafuta safi. Ndizo Sulemani alizompa Hiramu mwaka kwa mwaka. 12#1 Fal 3:12; 2 Nya 1:12; Yak 1:5 BWANA akampa Sulemani hekima, kama alivyomwahidia. Ikawa amani kati yao Hiramu na Sulemani; wakafanya mikataba kati yao wawili.
13Mfalme Sulemani akakusanya kutoka kila mahali katika Israeli watu wa shokoa nao walikuwa elfu thelathini. 14#1 Fal 12:18 Akatuma watu elfu kumi huko Lebanoni kwa zamu kila mwezi. Mwezi mmoja walikaa huko Lebanoni na miezi miwili walikuweko nyumbani kwao. Na Adoramu alikuwa msimamizi wa shokoa. 15Sulemani alikuwa na wapagazi elfu sabini na wakatao miti milimani elfu themanini; 16mbali na maafisa wake Sulemani waliokuwa wakuu wa kazi wa watu elfu tatu waliotenda kazi. 17Mfalme akaamuru, nao wakaleta mawe makubwa, mawe ya thamani, ili wauweke msingi wa nyumba kwa mawe yaliyochongwa. 18Na waashi wa Sulemani na waashi wa Hiramu na Wagebali wakayachonga, wakaweka tayari miti na mawe ya kuijenga nyumba.

Currently Selected:

1 Wafalme 5: SRUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy