YouVersion Logo
Search Icon

1 Wafalme 4

4
Maofisa tawala wa Sulemani
1Basi mfalme Sulemani akawa mfalme juu ya Israeli wote. 2Na hawa ndio wakuu aliokuwa nao; Azaria mwana wa Sadoki, kuhani, 3#2 Sam 8:16 Elihorefu na Ahiya, wana wa Shausha, waandishi; Yehoshafati mwana wa Ahiludi mwenye kuandika tarehe;#4:3 Au, mkumbushi. 4#1 Fal 2:35; 2:27 na Benaya mwana wa Yehoyada alikuwa jemadari wa jeshi; na Sadoki na Abiathari walikuwa makuhani; 5#2 Sam 8:18; 20:26; 15:37; 16:16; 1 Nya 27:33 na Azaria mwana wa Nathani alikuwa afisa mkuu tawala; na Zabudi mwana wa Nathani alikuwa kuhani, rafiki yake mfalme. 6#1 Fal 5:14 Na Ahishari alikuwa mkuu wa kasri; na Adoramu mwana wa Abda alikuwa msimamizi wa shokoa. 7Sulemani alikuwa na maafisa tawala kumi na wawili juu ya Israeli wote, walioleta chakula cha mfalme na nyumba yake; kila mtu alikuwa na mwezi mmoja katika mwaka kuleta chakula. 8Na haya ndiyo majina yao. Mwana wa Huri, mlimani mwa Efraimu. 9Mwana wa Dekari, kutoka Makasi, na Shaalbimu na Beth-shemeshi na Elon-beth-hanani. 10Mwana wa Hesedi, katika Arubothi; na Soko ilikuwa kwake na nchi yote ya Heferi. 11Mwana wa Abinadabu katika Nafath-dori yote; ndiye aliyekuwa naye Tafathi binti Sulemani kuwa mke wake. 12Baana mwana wa Ahiludi, katika Taanaki na Megido, na Beth-sheani yote, iliyo kando ya Sarethani, chini ya Yezreeli, tangu Beth-sheani mpaka Abel-mehola, hata kupita Yokmeamu. 13#Hes 32:41; Kum 3:4 Mwana wa Geberi katika Ramoth-gileadi; na kwake ilikuwa miji ya Yairi mwana wa Manase iliyomo Gileadi; na kwake ilikuwa wilaya ya Argobu, iliyomo Bashani, miji mikubwa sitini yenye kuta na makomeo ya shaba. 14Ahinadabu mwana wa Ido, katika Mahanaimu. 15Ahimaasi, katika Naftali; naye ndiye aliyemwoa Basemathi binti Sulemani. 16Baana mwana wa Hushai, katika Asheri na Bealothi. 17Yehoshafati mwana wa Parua, katika Isakari. 18Shimei mwana wa Ela, katika Benyamini. 19#Kum 3:8 Geberi mwana wa Uri, katika nchi ya Gileadi, nchi ya Sihoni mfalme wa Waamori, na Ogu mfalme wa Bashani; naye alikuwa mkuu pekee katika nchi hiyo.
Utukufu wa utawala wa Sulemani
20 # Mwa 22:17; 1 Fal 3:8; Mit 14:28; 1 Sam 30:16; 1 Nya 12:39; Ayu 1:18; Zab 72:3; Mik 4:4; Zek 9:15; Mdo 2:46 Yuda na Israeli walikuwa wengi kama mchanga wa pwani kwa wingi, wakila, na kunywa, na kufurahi.
21 # Mwa 15:18; Kut 23:31; Kum 11:24; Yos 1:4; 2 Nya 9:26; Zab 72:8 Sulemani akatawala juu ya falme zote, toka Mto mpaka nchi ya Wafilisti, na hata mpaka wa Misri; walimletea tunu, na kumtumikia Sulemani siku zote za maisha yake.
22Na vyakula vya Sulemani vya siku moja vilikuwa kori#4:22 Kori ni kipimo cha Kiebrania cha kadiri lita 220. thelathini za unga mzuri, na kori sitini za ngano, 23na ng'ombe kumi walionona, na ng'ombe ishirini za malisho, na kondoo mia moja, pamoja na ayala, na paa, na kulungu, na kuku walionona. 24#Mwa 10:19 Kwani alikuwa akitawala nchi yote upande huu wa Mto, toka Tifsa mpaka Gaza, juu ya wafalme wote wa upande huu wa Mto; naye alikuwa na amani pande zake zote. 25#Kum 33:28,29; Zab 33:12; 144:12-15; Yer 23:6; Mik 4:4; Zek 3:10 Yuda na Israeli wakakaa salama, kila mtu chini ya mzabibu wake na chini ya mtini wake, tokea Dani mpaka Beer-sheba, siku zote za Sulemani.
26 # Kum 17:16; 1 Fal 10:25,26; 2 Nya 9:25; Zab 20:7 Tena Sulemani alikuwa na mabanda ya farasi elfu arubaini kwa magari yake, na wapandao farasi elfu kumi na mbili. 27Na maofisa wale wakaleta chakula kwa mfalme Sulemani na kwa wote walioijia meza ya mfalme Sulemani, kila mtu katika mwezi wake, kisipunguke kitu. 28#Est 8:14; Mik 1:13 Shayiri pia na majani kwa farasi, na kwa wanyama wenye mbio, wakaleta mahali walipokuwapo, kila mtu kwa kadiri ya kazi yake.
Sifa za hekima ya Sulemani
29Mungu akampa Sulemani hekima, na akili nyingi sana, na moyo mkuu, kama mchanga ulioko pwani. 30#Mwa 25:6; Ayu 28:28; Mit 2:1; Mdo 7:22 Hekima ya Sulemani ikapita hekima ya watu wote#4:30 Katika Kiebrania ni wana wote. wa mashariki, na hekima zote za Misri. 31#1 Nya 15:19; 6:33 Kwa kuwa alikuwa na hekima kuliko watu wote; kuliko Ethani Mwezrahi, na Hemani, na Kalkoli, na Darda, wana wa Maholi; zikaenea sifa zake kati ya mataifa yote yaliyozunguka. 32#Mit 1:1; Mhu 12:9; Wim 1:1 Naye akanena mifano elfu tatu, na nyimbo zake zilikuwa elfu moja na tano. 33Akanena habari za miti tangu mwerezi ulioko Lebanoni hata hisopo umeao ukutani; pia akanena habari za wanyama, na za ndege, na vitambaavyo, na samaki. 34#1 Fal 10:1; 2 Nya 9:1 Watu wakaja kutoka mataifa yote, toka wafalme wote wa ulimwengu, waliokuwa wamepata habari za hekima yake, ili waisikie hekima ya Sulemani.

Currently Selected:

1 Wafalme 4: SRUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy