YouVersion Logo
Search Icon

Zab 111

111
Sifa kwa Maajabu ya Mungu
1Haleluya#111:1Haleluya maana yake ni, Msifuni BWANA..
Nitamshukuru BWANA kwa moyo wangu wote,
Barazani pa wanyofu wa moyo na katika mkutano.
2 # Ayu 38:1 Matendo ya BWANA ni makuu,
Yafikiriwa sana na wapendezwao nayo.
3Kazi yake ni heshima na adhama,
Na haki yake yakaa milele.
4Amefanya ukumbusho wa matendo yake ya ajabu;
BWANA ni mwenye fadhili na rehema.
5Amewapa wamchao chakula;
Atalikumbuka agano lake milele.
6Amewajulisha watu wake uwezo wa matendo yake,
Kwa kuwapa urithi wa mataifa.
7 # Zab 19:7 Matendo ya mikono yake ni kweli na hukumu,
Maagizo yake yote ni amini,
8 # Ufu 15:3 Yamethibitika milele na milele,
Yamefanywa katika kweli na adili.
9Amewapelekea watu wake ukombozi,
Ameamuru agano lake liwe la milele,
Jina lake ni takatifu la kuogopwa.
10 # Kum 4:6; Ayu 28:28; Mit 1:7; 9:10; Mhu 12:3 Kumcha BWANA ndio mwanzo wa hekima,
Wote wafanyao hayo wana akili njema,
Sifa zake zakaa milele.

Currently Selected:

Zab 111: SUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in