YouVersion Logo
Search Icon

Zab 108

108
Sifa na Sala ya Ushindi
Wimbo. Zaburi ya Daudi.
1Ee Mungu, moyo wangu u thabiti,
Nitaimba, nitaimba zaburi,
Naam, kwa utukufu wangu.
2Amka, kinanda na kinubi,
Nitaamka alfajiri.
3Ee BWANA, nitakushukuru kati ya watu,
Nitakuimbia zaburi kati ya mataifa.
4 # Mik 7:18-20; Hes 14:18; Kum 7:9; Zab 36:5 Maana fadhili zako ni kubwa hata mbinguni,
Na uaminifu wako hata mawinguni.
5 # Zab 57:5 Ee Mungu, utukuzwe juu ya mbingu,
Na juu ya nchi yote uwe utukufu wako.
6Ili wapenzi wako waopolewe,
Uokoe kwa mkono wako wa kuume, uniitikie.
7Mungu amenena kwa utakatifu wake,
Nami nitashangilia.
Nitaigawanya Shekemu,
Nitalipima bonde la Sukothi.
8 # Mwa 49:10 Gileadi ni yangu, na Manase ni yangu,
Na Efraimu ni nguvu ya kichwa changu.
Yuda ni fimbo yangu ya kifalme,
9Moabu ni bakuli langu la kunawia.
Nitamtupia Edomu kiatu changu,
Na kumpigia Filisti kelele za vita.
10 # Zab 60:9 Ni nani atakayenipeleka hata mji wenye boma?
Ni nani atakayeniongoza hata Edomu?
11Ee Mungu, si Wewe uliyetutupa?
Wala, Ee Mungu, hutoki na majeshi yetu?
12Utuletee msaada juu ya mtesi,
Maana wokovu wa binadamu haufai.
13 # Isa 25:10; 30:3; Omb 1:15; Mal 4:3; Mdo 1:20; Ufu 14:19-20 Kwa msaada wa Mungu tutatenda makuu,
Maana Yeye atawakanyaga watesi wetu.

Currently Selected:

Zab 108: SUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in