YouVersion Logo
Search Icon

Omb 5

5
Ombi la Kuhurumiwa
1Ee BWANA, kumbuka yaliyotupata;
Utazame na kuiona aibu yetu.
2Urithi wetu umegeuka kuwa mali ya wageni;
Na nyumba zetu kuwa mali ya makafiri.
3Tumekuwa yatima waliofiwa na baba;
Mama zetu wamekuwa kama wajane.
4Tumekunywa maji yetu kwa fedha;
Kuni zetu twauziwa.
5Watufuatiao wa juu ya shingo zetu;
Tumechoka tusipate raha yo yote.
6 # Mwa 24:2; Yer 50:15; Hos 12:1 Tumewapa hao Wamisri mkono;
Na Waashuri nao, ili tushibe chakula.
7 # Yer 16:12; Eze 18:2; Mt 23:32 Baba zetu walitenda dhambi hata hawako;
Na sisi tumeyachukua maovu yao.
8Watumwa wanatutawala;
Hakuna mtu wa kutuokoa na mikono yao.
9Twapata chakula kwa kujihatarisha nafsi zetu;
Kwa sababu ya upanga wa nyikani.
10Ngozi yetu ni nyeusi kama tanuu;
Kwa sababu ya hari ya njaa ituteketezayo.
11 # Isa 13:16 Huwatia jeuri wanawake katika Sayuni;
Na mabikira katika miji ya Yuda.
12Wakuu hutungikwa kwa mikono yao;
Nyuso za wazee hazipewi heshima.
13 # Amu 16:21 Vijana huyachukua mawe ya kusagia;
Na watoto hujikwaa chini ya kuni.
14 # 2 Fal 25:18 Wazee wameacha kwenda langoni;
Na vijana kwenda ngomani.
15Furaha ya mioyo yetu imekoma;
Machezo yetu yamegeuka maombolezo.
16Taji ya kichwa chetu imeanguka;
Ole wetu! Kwa kuwa tumetenda dhambi.
17 # Ayu 17:7; Zab 6:7 Kwa sababu hiyo mioyo yetu imezimia;
Kwa ajili ya hayo macho yetu hayaoni vema.
18Kwa ajili ya mlima Sayuni ulio ukiwa,
Mbweha hutembea juu yake.
19Wewe, BWANA, unadumu milele;
Kiti chako cha enzi ni tangu kizazi hata kizazi.
20Mbona watusahau sikuzote;
Na kutuacha muda huu mwingi?
21Ee BWANA, utugeuze kwako, nasi tutageuka; Zifanye mpya siku zetu kama siku za kale.
22Isipokuwa wewe umetukataa kabisa;
Nawe una hasira nyingi sana juu yetu.

Currently Selected:

Omb 5: SUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in