YouVersion Logo
Search Icon

Omb 4

4
Adhabu ya Sayuni
1Jinsi dhahabu ilivyoacha kung’aa,
Na dhahabu iliyo safi ilivyobadilika!
Mawe ya patakatifu yametupwa
Mwanzo wa kila njia.
2 # 2 Kor 4:7 Wana wa Sayuni wenye thamani,
Walinganao na dhahabu safi,
Jinsi wanavyodhaniwa kuwa vyombo vya udongo,
Kazi ya mikono ya mfinyanzi!
3 # Ayu 39:14 Hata mbwa-mwitu hutoa matiti,
Huwanyonyesha watoto wao;
Binti ya watu wangu amekuwa mkali,
Mfano wa mbuni jangwani.
4 # Zab 22:15 Ulimi wa mtoto anyonyaye
Wagandamana na kaakaa lake kwa kiu;
Watoto wachanga waomba chakula,
Wala hakuna hata mmoja awamegeaye.
5 # Ayu 24:8; Lk 15:16 Wale waliokula vitu vya anasa
Wameachwa peke yao njiani;
Wale waliokuzwa kuvaa nguo nyekundu
Wakumbatia jaa.
6 # Mwa 19:24 Maana uovu wa binti ya watu wangu ni mkubwa
Kuliko dhambi ya Sodoma,
Uliopinduliwa kama katika dakika moja,
Wala mikono haikuwekwa juu yake.
7Wakuu wake walikuwa safi kuliko theluji,
Walikuwa weupe kuliko maziwa;
Miili yao, walikuwa wekundu kuliko marijani,
Na umbo lao kama yakuti samawi.
8 # Zab 102:5 Nyuso zao ni nyeusi kuliko makaa;
Hawajulikani katika njia kuu;
Ngozi yao yagandamana na mifupa yao
Imekauka, imekuwa kama mti.
9Heri wale waliouawa kwa upanga
Kuliko wao waliouawa kwa njaa;
Maana hao husinyaa, wakichomwa
Kwa kukosa matunda ya mashamba.
10 # Omb 2:20; Kum 28:57; Eze 5:10 Mikono ya wanawake wenye huruma
Imewatokosa watoto wao wenyewe;
Walikuwa ndio chakula chao
Katika uharibifu wa binti ya watu wangu.
11 # Kum 32:22 BWANA ameitimiza kani yake,
Ameimimina hasira yake kali;
Naye amewasha moto katika Sayuni
Ulioiteketeza misingi yake.
12 # Kum 29:24 Wafalme wa dunia hawakusadiki,
Wala wote wakaao duniani,
Ya kwamba mtesi na adui wangeingia
Katika malango ya Yerusalemu.
13 # Yer 5:31; Mt 23:31 Ni kwa sababu ya dhambi za manabii wake
Na maovu ya makuhani wake,
Walioimwaga damu ya wenye haki
Katikati yake.
14 # Yer 2:34 Hutanga-tanga njiani kama vipofu,
Wametiwa unajisi kwa damu;
Hata ikawa watu wasiweze
Kuyagusa mavazi yao.
15Watu waliwapigia kelele, Ondokeni, Uchafu,
Ondokeni, ondokeni, msiguse;
Walipokimbia na kutanga-tanga, watu walisema kati ya mataifa,
Hawatakaa hapa tena.
16 # Omb 5:12 Hasira ya BWANA imewatenga,
Yeye hatawaangalia tena;
Hawakujali nafsi za wale makuhani,
Hawakuwaheshimu wazee wao.
17 # 2 Fal 24:7; Isa 20:5,6 Macho yetu yamechoka
Kwa kuutazamia bure msaada wetu;
Katika kungoja kwetu tumengojea taifa
Lisiloweza kutuokoa.
18 # 2 Fal 25:4; Yer 51:33 Wanatuvizia hatua zetu,
Hata hatuwezi kwenda katika njia zetu;
Mwisho wetu umekaribia, siku zetu zimetimia;
Maana mwisho wetu umefika.
19Waliotufuatia ni wepesi
Kuliko tai za mbinguni;
Hao walitufuatia milimani,
Nao walituotea jangwani.
20 # Mwa 2:7; Yer 52:9 Pumzi ya mianzi ya pua zetu, masihi#4:20 Au, mtiwa mafuta (taz. 1 Sam 2:10). wa BWANA,
Alikamatwa katika marima yao;
Ambaye kwa habari zake tulisema,
Chini ya kivuli chake tutakaa kati ya mataifa.
21Furahi, ushangilie, Ee binti Edomu,
Ukaaye katika nchi ya Usi;
Hata kwako kikombe kitapita,
Utalewa, na kujifanya uchi.
22Uovu wako umetimia, Ee binti Sayuni;
Hatakuhamisha tena;
Atapatiliza uovu wako, Ee binti Edomu;
Atazivumbua dhambi zako.

Currently Selected:

Omb 4: SUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in