YouVersion Logo
Search Icon

Kum 13

13
1 # 2 The 2:9 Kukizuka katikati yako nabii, au mwotaji wa ndoto, akikutolea ishara au ajabu, 2#Yer 28:9; Mt 7:22ikatukia hiyo ishara au hiyo ajabu aliyokuambia akisema, Na tuifuate miungu mingine usiyoijua, tuitumikie hiyo; 3#Mt 24:24; 1 Kor 11:19; 2 The 2:11; Ufu 13:14wewe usiyasikize maneno ya nabii yule, au yule mwotaji wa ndoto, kwa kuwa BWANA, Mungu wenu, yuawajaribu, apate kujua kwamba mwampenda BWANA, Mungu wenu, kwa mioyo yenu yote na roho zenu zote. 4#2 Fal 23:3; 2 Nya 34:31; 1 Yoh 1:7; 2 Yoh 1:6Tembeeni kwa kumfuata BWANA, Mungu wenu; mcheni na kushika maagizo yake na kuisikia sauti yake, nanyi mtumikieni na kushikamana naye. 5#1 Fal 18:40; Isa 9:15,16; Yer 14:15; Zek 13:3; Ufu 19:20; 2 Fal 10:18-28; 1 Kor 5:13Na yule nabii, au yule mwotaji wa ndoto, na auawe, kwa kuwa amesema yaliyopotoka juu ya BWANA, Mungu wenu, aliyewatoa katika nchi ya Misri, akakukomboa katika nyumba ya utumwa, apate yule mtu kukupotoa katika njia aliyokuamuru BWANA, Mungu wako, uiendee. Ndivyo utakavyouondoa uovu utoke katikati yako.
6 # Ayu 2:9; Mik 7:5 Atakapokushawishi kwa siri ndugu yako, mwana wa mamaako, au mwana wako, au binti yako, au mke wa kifuani mwako, au rafiki yako aliye kama moyo wako, akikuambia, Twende tukaabudu miungu mingine usiyoijua wewe wala baba zako; 7katika miungu ya mataifa yaliyo kando-kando yenu karibu nawe au mbali nawe, tokea ncha moja ya dunia hata ncha ya pili ya dunia; 8#Kut 20:3; Mit 1:10; Gal 1:8,9; 1 Yoh 5:21usimkubalie wala usimsikize; wala jicho lako lisimwonee huruma, wala usimwache, wala usimfiche; 9#Kum 17:7; Mdo 7:58mwue kweli; mkono wako na uwe wa kwanza juu yake katika kumwua, na baadaye mikono ya watu wote. 10Nawe mtupie mawe hata afe; kwa kuwa alitaka kukupotoa na BWANA, Mungu wako aliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa. 11#Kum 19:20Na Israeli wote watasikia na kuogopa, wasifanye tena uovu mfano wa huo katikati yako.
12 # Yos 22:11; Amu 20:1 Ukisikia yasemwa habari ya miji yako mmojawapo, akupayo BWANA, Mungu wako, ukae humo, ukiambiwa, 13#1 Sam 2:12; 2 Kor 6:15; 1 Yoh 2:19; Yud 1:19; 2 Fal 17:21Kumetoka katikati yako mabaradhuli kadha wa kadha, wamewapotoa wenyeji wa mji wao, wakisema, Twendeni tukaabudu miungu mingine msiyoijua; 14ndipo nawe uulize na kutafuta, ukiuliza kwa bidii; nawe angalia, ikiwa kweli, na jambo lile halina shaka, kwamba machukizo mfano wa haya yafanyika katikati yako; 15#Yos 6:17hakika yako uwapige wenyeji wa mji ule kwa makali ya upanga, kwa kuwaangamiza kabisa, pamoja na vitu vyote vilivyomo, na wanyama walio humo, kwa makali ya upanga. 16#Yos 8:28; Isa 17:1; 25:2; Yer 49:2Na nyara zake zote uzikusanyie katikati ya njia yake; na mji uuteketeze kwa moto, na nyara zake zote, kuwe sadaka kamili ya kuteketezwa kwa BWANA, Mungu wako; nao utakuwa magofu milele; usijengwe tena. 17#Kum 7:26; Yos 6:18; 7:1,11,12; 6:26; Mwa 22:17; 26:4,24Kisishikamane na mkono wako kitu cho chote katika kitu kilichoharimishwa; ili ageuke BWANA na ukali wa hasira zake akurehemu, akuonee huruma, na kukufanya kuwa wengi, kama alivyowaapia baba zako; 18#Kum 12:25; Mt 6:33; 7:21,24utakaposikiza sauti ya BWANA, Mungu wako kwa kushika maagizo yake yote nikuagizayo leo, ufanye yaliyoelekea machoni pa BWANA, Mungu wako.

Currently Selected:

Kum 13: SUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy