YouVersion Logo
Search Icon

Kum 12

12
Kubomolewa kwa Madhabahu ya Miungu
1 # Kum 4:10; 1 Fal 8:40; Gal 6:9 Hizi ndizo amri na hukumu mtakazotunza kuzifanya katika nchi aliyokupa BWANA, Mungu wa baba zako, uimiliki, siku zote mtakazoishi juu ya nchi. 2#Kut 34:33; 2 Fal 16:4; 17:10,11; Yer 3:6Vunjeni kabisa mahali pote walipokuwa wakiitumikia miungu yao mataifa mtakayoyamiliki, juu ya milima mirefu, na juu ya vilima, na chini ya kila mti wenye majani mabichi; 3#Kum 7:5; Hes 33:52; Amu 2:2; Kut 23:13; Zab 16:4; Zek 13:2nanyi zivunjeni madhabahu zao, zibomoeni nguzo zao, na maashera yao yateketezeni kwa moto, na sanamu za kuchonga za miungu yao zikateni; na jina lao lifutilieni mbali na mahali hapo. 4Wala msimfanyie hivyo BWANA, Mungu wenu. 5#Kum 26:2; Yos 9:27; 1 Fal 8:29; 2 Nya 7:12; Zab 78:68Lakini mahali atakapochagua BWANA, Mungu wenu, katika kabila zenu zote, apaweke jina lake, maana, ni makao yake, elekezeni nyuso zenu hapo, nawe wende huko; 6#Law 17:3; Kum 14:22pelekeni huko sadaka zenu za kuteketezwa, na dhabihu zenu, na zaka zenu, na sadaka ya kuinuliwa ya mikono yenu, na nadhiri zenu, na sadaka zenu za hiari, na wazaliwa wa kwanza wa makundi yenu ya ng’ombe na ya kondoo; 7#Kum 14:26; Law 23:40; Mhu 3:12; 5:18na huko mtakula mbele za BWANA, Mungu wenu, nanyi furahini katika yote mtakayotia mikono yenu, ninyi na wa nyumbani mwenu, aliyokubarikia BWANA, Mungu wako. 8Msifanye kwa kufuata mambo yote tuyafanyayo hapa leo, kila mtu kama aonavyo vema machoni pake; 9kwani hamjafikilia bado katika raha na urithi akupao BWANA, Mungu wako.
10Lakini mtakapovuka Yordani na kukaa katika nchi anayowarithisha BWANA, Mungu wenu, akawapeni raha, akiwaokoa na adui zenu pande zote, mkakaa salama; 11#Kum 14:23; 15:20; 16:2; Yos 18:1; 1 Fal 8:29; Zab 78:68; 87:2wakati huo itakuwa kwamba mahali pale atakapopachagua BWANA, Mungu wenu, alikalishe jina lake, hapo ndipo mtakapoleta kila kitu ninachowaamuru; sadaka zenu za kuteketezwa, na dhabihu zenu, na zaka zenu, na sadaka ya kuinuliwa ya mikono yenu, na nadhiri zenu zote teule mtakazoweka kwa BWANA. 12#Kum 10:9; 14:29Nanyi mtafurahi mbele za BWANA, Mungu wenu, ninyi, na wana wenu, na binti zenu, na watumishi wenu wanawaume na wanawake, na Mlawi aliyemo malangoni mwenu; kwa kuwa hana sehemu wala urithi kwenu.
Maagizo ya Mahali pa Kuabudu
13 # Law 17:4 Ujihadhari usitoe sadaka zako za kuteketezwa katika kila mahali upaonapo; 14bali katika mahali atakapopachagua BWANA katika kabila zako mojawapo, ndipo utakapotoa sadaka zako za kuteketezwa, ndipo utakapotenda yote nikuamuruyo. 15#Mwa 9:3; Kum 14:5; 15:22Pamoja na haya waweza kuchinja nyama na kula ndani ya malango yako yote, kwa kufuata yote yatamaniwayo na roho yako, kwa mfano wa baraka ya BWANA, Mungu wako, aliyokupa; aliye tohara na asiye tohara ana ruhusa kula katika nyama hiyo, kama ya paa na ya kulungu. 16#Mwa 9:4; Law 7:26-27; 17:10-14; 19:26; Kum 15:23; 1 Sam 14:33,34; Mdo 15:20,29Lakini msiile damu; imwageni juu ya nchi kama maji. 17Usile ndani ya malango yako zaka ya nafaka zako, wala ya divai yako, wala ya mafuta yako, wala wazaliwa wa kwanza wa makundi yako, ya ng’ombe wala ya kondoo, wala nadhiri zako uwekazo zo zote, wala sadaka zako za hiari, wala sadaka ya kuinuliwa ya mkono wako; 18#Kum 14:23; Mhu 3:12,13; 5:18-20lakini hivyo mtakula mbele za BWANA, Mungu wako, mahali atakapochagua BWANA, Mungu wako, wewe, na mwanao mume na mke, na mtumwa wako mume na mke, na Mlawi aliye ndani ya malango yako; nawe furahi mbele za BWANA, Mungu wako, katika yote utakayotia mkono wako. 19#Kum 14:27Jilinde nafsi yako usimwache Mlawi siku zote uishizo katika nchi yako.
20 # Mwa 15:18; 28:14; Kut 34:24; Kum 11:24; 19:8 BWANA, Mungu wako, atakapoongeza mpaka wako, kama alivyokuahidi, nawe utakaposema, Nataka kula nyama, kwa kuwa roho yako yatamani kula nyama; waweza kula nyama, kwa kufuata yote inayotamani roho yako. 21Na mahali atakapochagua BWANA, Mungu wako, apaweke jina lake, pakiwa mbali nawe mno, ndipo utakapochinja katika kundi lako la ng’ombe na kondoo alilokupa BWANA kama nilivyokuagiza, nawe utakula ndani ya malango yako, kwa kufuata yote inayotamani roho yako. 22Kama vile aliwavyo paa na kulungu, ndivyo utakavyoila nyama hii; asiyekuwa tohara na aliye tohara wataila pia. 23#Law 17:10-14; Mwa 9:4Ila ujihadhari kwamba usile damu, kwani ile damu ndiyo uhai; na uhai usile pamoja na nyama. 24Usiile; imwage juu ya nchi kama maji. 25#Kum 4:40; Isa 3:10; Kut 15:26; Kum 13:18; 1 Fal 11:38Usiile; ili upate kufanikiwa, na watoto wako baada yako utakapofanya yaliyoelekea machoni pa BWANA. 26#Hes 5:9,10; 18:19; 1 Nya 21:22,24Ila vitu vyako vitakatifu ulivyo navyo, na nadhiri zako, uvitwae ukaende mahali atakapochagua BWANA; 27#Law 1:5-13; 17:11nawe zisongeze sadaka zako za kuteketezwa, nyama na damu, juu ya madhabahu ya BWANA, Mungu wako; na damu ya dhabihu zako uimwage juu ya madhabahu ya BWANA, Mungu wako, na wewe utakula nyama yake. 28#Zab 25:12,13; Mit 1:33; 3:1-4; Mhu 8:12Maneno haya nikuagizayo yote yatunze na kuyasikiza, ili upate kufanikiwa na watoto wako baada yako milele, hapo uyafanyapo yaliyo mema na kuelekea machoni pa BWANA, Mungu wako.
Onyo dhidi ya Kuabudu Sanamu
29 # Kut 23:23; Yos 23:4; Zab 78:55 BWANA, Mungu wako, atakapoyakatilia mbali hayo mataifa mbele yako, huko uingiako kuyamiliki, nawe ukawatwaa, na kuketi katika nchi yao; 30ujiangalie, usije ukanaswa ukawafuata, wakiisha kuangamizwa mbele yako; wala usije ukauliza habari za miungu yao, ukisema, Mataifa haya waitumikiaje miungu yao? Nami nifanye vivyo. 31#Law 18:3,26-30; 2 Fal 17:15; 2 Nya 33:2; 36:14; Yer 32:35Usimtende kama haya BWANA, Mungu wako; kwani kila yaliyo machukizo kwa BWANA, ayachukiayo yeye, wameifanyia miungu yao; kwa maana hata wana wao na binti zao huiteketezea hiyo miungu yao ndani ya moto.
32 # Kum 4:2; Ufu 22:18-19; Yos 1:7; Mit 30:6 Neno niwaagizalo lo lote liangalieni kulifanya; usiliongeze, wala usilipunguze.

Currently Selected:

Kum 12: SUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy