YouVersion Logo
Search Icon

1 Sam 19

19
Yonathani Amtetea Daudi
1 # Mit 27:4 Kisha Sauli akasema na mwanawe Yonathani, tena na watumishi wake wote, kwamba wamwue Daudi. 2#Mdo 23:16Lakini huyo Yonathani, mwana wake Sauli, alikuwa akipendezwa sana na Daudi. Basi Yonathani akamwambia Daudi, akasema, Sauli, baba yangu, anatafuta kukuua; basi, nakusihi, ujiangalie sana asubuhi, ukae mahali pa siri na kujificha; 3na mimi nitatoka nje na kusimama kando ya babangu huko shambani ulipo wewe, nami nitazungumza na babangu habari zako; nami nikiona neno lo lote nitakuambia. 4#Mit 31:8; Mwa 42:22; 1 Sam 2:25; 2 Nya 6:22; Zab 35:12; 109:5; Mit 17:13; Yer 18:20; 1 Kor 8:12; 1 Yoh 3:15Naye Yonathani akamsifu Daudi kwa Sauli, babaye akamwambia, Mfalme asikose juu ya mtumishi wake, yaani, juu ya Daudi kwa maana yeye hakukosa juu yako, tena matendo yake kwako yamekuwa mema sana. 5#Amu 9:17; 12:3; 1 Sam 28:21; Zab 119:109; 1 Sam 17:49; 11:13; 1 Nya 11:14; 1 Sam 20:32; Mt 27:4Kwa kuwa alitia uhai wake mkononi mwake, na kumpiga yule Mfilisti, naye BWANA akawatendea Israeli wote wokovu mkuu. Wewe mwenyewe uliona jambo hilo, ukafurahi; basi kwa nini kukosa juu ya damu isiyo na hatia, umwue huyo Daudi bure? 6Sauli akaisikiliza sauti ya Yonathani; naye Sauli akaapa, Aishivyo BWANA, yeye hatauawa. 7Basi Yonathani akamwita Daudi, naye Yonathani akamjulisha mambo hayo yote. Kisha Yonathani akamleta Daudi kwa Sauli, naye alikuwa akihudhuria mbele yake, kama kwanza.
Mikali Amsaidia Daudi Kumtoroka Sauli
8Baada ya hayo kulikuwa na vita tena; naye Daudi akatoka, naye akapigana na Wafilisti, naye akawaua kwa uuaji mkuu; nao wakakimbia mbele yake.
9 # 1 Sam 16:14; 18:10 Tena ikawa, roho mbaya kutoka kwa BWANA ilimjilia Sauli, hapo alipoketi ndani ya nyumba yake, akiwa na mkuki wake mkononi mwake; naye Daudi alikuwa akipiga kinubi kwa mkono wake. 10#Ayu 5:2; Zab 5:6; Mit 1:16; 29:10Sauli akajaribu kumpiga Daudi hata ukutani kwa mkuki wake, ila yeye akaponyoka kutoka mbele ya Sauli, nao huo mkuki akaupiga ukutani; naye Daudi akakimbia, akaokoka usiku ule. 11#Zab 59:1Kisha Sauli akatuma wajumbe mpaka nyumbani kwa Daudi, ili wamvizie na kumwua asubuhi; naye Mikali, mkewe Daudi, akamwambia, akasema, Wewe usipojiponya nafsi yako usiku huu, kesho utauawa. 12#Yos 2:15; Mdo 9:24,25; 2 Kor 11:32,33Basi Mikali akamtelemsha Daudi dirishani; naye akaenda akakimbia na kuokoka. 13#Mwa 31:19; Amu 17:5Ndipo Mikali akakitwaa kinyago, na kukilaza kitandani, akatia na mto wa singa za mbuzi kichwani pake, na kukifunika kwa nguo. 14Naye Sauli alipotuma wajumbe ili kumkamata Daudi, yeye alisema, Hawezi. 15Basi Sauli akawatuma hao wajumbe ili wamtazame Daudi, akisema, Mleteni kwangu juu ya kitanda chake, nipate kumwua. 16Nao wajumbe walipoingia, kumbe! Kuna kinyago kitandani, na mto wa singa za mbuzi kichwani pake! 17#2 Sam 2:22Sauli akamwambia Mikali, Mbona wewe umenidanganya hivi, na kumwacha adui yangu aende, hata ameniponyoka? Naye Mikali akamjibu Sauli, Yeye aliniambia, Niache niende zangu; kwa nini nikuue?
Daudi na Samweli wakiwa Rama
18 # Mit 17:17; Mal 2:7 Hivyo Daudi akakimbia, akajiponya, akamwendea Samweli huko Rama, akamwambia hayo yote Sauli aliyomtenda. Kisha yeye na Samweli wakaenda na kukaa katika Nayothi. 19Naye Sauli akaambiwa, kusema, Angalia, yule Daudi yuko katika Nayothi, huko Rama. 20#Yn 7:32,45; 1 Sam 10:5,6; 1 Kor 14:3,24,25; Hes 11:25; Yoe 2:28Basi Sauli akatuma wajumbe ili kumkamata Daudi; nao hapo walipowaona jamaa ya manabii wakitabiri, na Samweli amesimama kama mkuu wao, roho ya Mungu ikawajilia wajumbe wa Sauli, nao pia wakatabiri. 21Naye Sauli alipoambiwa, alituma wajumbe wengine, wao nao wakatabiri. Naye Sauli akatuma wajumbe tena mara ya tatu, na wao pia wakatabiri. 22Kisha yeye mwenyewe akaenda Rama, akafika kunako kile kisima kikubwa kilicho huko Seku; akauliza, akasema, Je! Wako wapi Samweli na Daudi? Na mtu mmoja akajibu, Tazama, wako Nayothi, huko Rama. 23#Mwa 31:24; Hes 23:5; 24:2; 1 Sam 10:10; Mit 21:1; Dan 4:35; Mt 7:22; Yn 11:51; 1 Kor 13:2Basi akaenda Nayothi huko Rama, na roho ya Mungu ikamjilia yeye naye, akaendelea mbele, huku anatabiri, mpaka kufika Nayothi huko Rama. 24#1 Sam 10:11-12; Isa 20:2; 2 Sam 6:14,20; Mik 1:8; Mdo 9:21Naye akavua nguo zake, akatabiri mbele ya Samweli, akalala uchi mchana kutwa na usiku kucha siku ile. Kwa hiyo watu husema, Je! Sauli pia yumo miongoni mwa manabii?

Currently Selected:

1 Sam 19: SUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in