YouVersion Logo
Search Icon

1 Sam 18

18
Agano la Yonathani na Daudi
1 # Mwa 44:30; 2 Sam 18:33; Kol 2:2; Kum 13:6; 1 Sam 19:2; 20:17; 2 Sam 1:26; Mit 18:24; Yn 15:17-19; 1 Yoh 3:12-14 Ikawa Daudi alipokwisha kusema na Sauli, roho ya Yonathani, ikaambatana na roho ya Daudi, Yonathani akampenda kama roho yake mwenyewe. 2#1 Sam 8:11; 14:52; 17:15Sauli akamtwaa siku ile, wala hakumwacha arudi tena nyumbani kwa baba yake. 3Nao Yonathani na Daudi wakaahidiana, kwa kuwa alimpenda kama roho yake mwenyewe. 4Ndipo Yonathani akalivua joho alilokuwa amelivaa, akampa Daudi, na mavazi yake, hata na upanga wake pia, na upinde wake, na mshipi wake. 5Basi Daudi akatoka kwenda kila mahali alikotumwa na Sauli, akatenda kwa akili; Sauli akamweka juu ya watu wa vita; jambo hili likawa jema machoni pa watu wote, na machoni pa watumishi wa Sauli pia.
6 # Kut 15:20; Amu 5:1,2; 11:34; Zab 68:25; 150:4; Yer 31:4 Hata ikawa, walipokuwa wakienda, hapo Daudi aliporudi baada ya kumwua yule Mfilisti, wanawake wakatoka katika miji yote ya Israeli, kwa kuimba na kucheza, ili kumlaki mfalme Sauli; wakatoka na matari, na shangwe, na vinanda. 7#1 Sam 21:11; 29:5; Kut 15:21; Amu 5:3; 2 Nya 5:13; Zab 24:1-10; Isa 5:1Nao wale wanawake wakaitikiana wakicheza, wakasema,
Sauli amewaua elfu zake,
Na Daudi makumi elfu yake.
8 # Mhu 4:4 Basi Sauli akaghadhibika sana, na maneno haya yakamchukiza; akasema, Wamempa Daudi makumi elfu, na mimi wamenipa elfu tu; kuna nini tena awezayo kupata, isipokuwa ni ufalme? 9#Mwa 4:5; 31:2,5; Mt 20:15; Lk 15:28Sauli akamwonea Daudi wivu tangu siku ile.
Sauli Ajaribu Kumwua Daudi
10 # 1 Sam 16:14; 19:24; 1 Fal 18:29; Mdo 16:16 Ikawa siku ya pili yake, roho mbaya kutoka kwa Mungu ikamjilia Sauli kwa nguvu, naye akatabiri ndani ya nyumba. Basi Daudi alikuwa akipiga kinubi kwa mkono wake kama siku zote; naye Sauli alikuwa na mkuki mkononi mwake. 11#1 Sam 19:10; 20:33; Mit 27:24Mara Sauli akautupa ule mkuki; maana alisema, Nitampiga Daudi hata ukutani. Daudi akaepa, akatoka mbele yake, mara mbili. 12#1 Sam 16:13; 28:15Sauli akamwogopa Daudi, kwa sababu BWANA alikuwa pamoja naye, ila amemwacha Sauli. 13#Hes 27:17; 2 Sam 5:2Kwa ajili ya hayo Sauli akamwondosha kwake, akamfanya awe akida wake juu ya askari elfu; naye akatoka na kuingia mbele ya watu. 14#Mwa 39:2; Yos 6:27; 1 Sam 10:7; 16:18; Mdo 7:9; 18:10Naye Daudi akatenda kwa busara katika njia zake zote naye BWANA alikuwa pamoja naye. 15Sauli alipoona ya kwamba alitenda kwa busara sana, yeye alimwogopa. 16Lakini Israeli wote na Yuda wakampenda Daudi; kwa kuwa alitoka na kuingia mbele yao.
Daudi Amwoa Mikali
17 # 1 Sam 17:25; Hes 32:20; 1 Sam 25:28; 2 Sam 12:9 Kisha Sauli akamwambia Daudi, Tazama, binti yangu mkubwa, Merabu, huyu nitakupa wewe ili umwoe; ila na wewe uniwie hodari wa vita, na kuvipiga vita vya BWANA. Maana Sauli alisema moyoni mwake, Mkono wangu usiwe juu yake, bali mkono wa Wafilisti na uwe juu yake. 18#Rut 2:10; 1 Sam 9:21; 2 Sam 7:18; Mit 15:33Naye Daudi akamwambia Sauli, Mimi ni nani, na jamaa zangu ni akina nani, au mbari ya babangu, katika Israeli, hata mimi niwe mkwewe mfalme? 19#2 Sam 21:8; Amu 7:22Lakini ikawa, wakati ule, ilipopasa Daudi apewe Merabu, binti Sauli, aliolewa na Adrieli, Mmeholathi.
20Walakini Mikali, binti Sauli, alimpenda Daudi; watu wakamwambia Sauli, na neno hilo likampendeza. 21#Kut 10:7; Zab 7:14-16; Mit 26:24-26; Yer 5:26; 9:8Naye Sauli akasema moyoni, Mimi nitamwoza huyu, awe mtego kwake, tena kwamba mkono wa Wafilisti uwe juu yake. Basi Sauli akamwambia Daudi mara ya pili, Leo utakuwa mkwe wangu. 22Naye Sauli akawaagiza watumishi wake, Zungumzeni na Daudi kwa siri, na kusema, Angalia, mfalme anakuridhia, na watumishi wake wote wanakupenda; haya basi! Na uwe mkwewe mfalme. 23Nao watumishi wa Sauli wakanena maneno hayo masikioni mwa Daudi. Daudi akasema, Je! Ninyi mwaona kuwa ni shani mimi kuwa mkwewe mfalme, nami ni maskini, tena sina cheo? 24Na hao watumishi wa Sauli wakampasha habari, wakisema, Ndivyo hivyo alivyosema Daudi. 25#Mwa 34:12; Kut 22:17; 1 Sam 14:24Naye Sauli akasema, Mwambieni Daudi hivi, Mfalme hataki mahari yo yote, ila anataka govi mia za Wafilisti, ili ajilipize kisasi adui za mfalme. Basi Sauli alidhani kumwangamiza Daudi kwa mkono wa Wafilisti. 26Na watumishi wake walipomwambia Daudi; maneno hayo, ilimpendeza Daudi sana kuwa mkwewe mfalme. Na siku zilikuwa hazijaisha bado; 27#2 Sam 3:14basi Daudi akainuka, akaenda yeye na watu wake, akaua katika Wafilisti watu mia mbili; na Daudi akazileta govi zao, wakampa mfalme hesabu kamili, ili awe mkwewe mfalme. Naye Sauli akamwoza Mikali, binti yake. 28Sauli akaona na kutambua ya kwamba BWANA alikuwa pamoja na Daudi; na huyo Mikali, binti Sauli, akampenda. 29#1 Sam 12:15; Ayu 5:2,12,13; Zab 37:12,13; Mhu 4:4; Yak 2:13Naye Sauli akazidi kumwogopa Daudi; Sauli akawa adui yake Daudi sikuzote.
30 # 2 Sam 11:1; Lk 21:15 Wakati huo wakuu wa Wafilisti wakatoka; kisha ikawa, kila mara walipotoka, Daudi akatenda kwa busara zaidi ya watumishi wote wa Sauli hivyo jina lake likawa na sifa kuu.

Currently Selected:

1 Sam 18: SUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in