YouVersion Logo
Search Icon

1 Nya 25

25
Waimbaji wa Hekaluni
1 # 1 Nya 12:28; 23:2; 6:33; 15:17; Kut 15:20; Hes 11:25; 1 Sam 10:5; 1 Nya 16:4; 23:5; Zab 150:3,5; 1 Kor 14:1; Ufu 15:2,4 Tena Daudi na maakida wa jeshi wakatenga kwa utumishi baadhi ya wana wa Asafu, na wa Hemani, na wa Yeduthuni, watakaotabiri kwa vinubi na vinanda, na matoazi; hii ndiyo hesabu ya wafanya kazi sawasawa na utumishi wao; 2wa wana wa Asafu; Zakuri, na Yusufu, na Nethania, na Asharela, wana wa Asafu; walioamriwa na Asafu, aliyetabiri kwa amri ya mfalme. 3Wa Yeduthuni; wana wa Yeduthuni; Gedalia, na Seri, na Yeshaya, na Hashabia, na Matithia, [na Shimei], watu sita; walioamriwa na baba yao Yeduthuni mwenye kinubi, aliyetabiri katika kumshukuru na kumsifu BWANA. 4Wa Hemani; wana wa Hemani; Bukia, Matania, Uzieli, Shebueli, na Yeremothi, Hanania, Hanani, Eliatha, Gidalti, na Romanti-ezeri, Yoshbekasha, Malothi, Hothiri, Mahaziothi; 5#1 Sam 9:9; 2 Sam 24:11; 1 Nya 21:9; 26:28; Amo 7:12; 1 Pet 4:11; Mwa 33:5; 1 Sam 1:17; 1 Nya 28:5; Zab 127:3; 128:3; Isa 3:18hao wote ndio wana wa Hemani, mwonaji wa mfalme, kwa maneno ya Mungu, ili kuinua pembe. Naye Mungu akampa Hemani wana kumi na wanne na binti watatu. 6Hao wote waliamriwa na baba yao, waimbe nyumbani mwa BWANA, wakiwa na matoazi, vinanda, na vinubi, kwa utumishi wa nyumba ya Mungu; Asafu, Yeduthuni, na Hemani wakiwa wanaamriwa na mfalme. 7#Zab 150:1; Efe 5:19; Kol 3:16; Yak 5:13Na hesabu yao, pamoja na ndugu zao waliofundishwa kumwimbia BWANA, wote waliokuwa wastadi, walikuwa mia mbili na themanini na wanane. 8#2 Nya 23:13Wakatupiwa kura ya ulinzi wao, sawasawa wote, mdogo kwa mkubwa, mwalimu kwa mwanafunzi. 9Kura ya kwanza ikamtokea Yusufu, kwa Asafu; ya pili Gedalia; yeye na nduguze na wanawe, kumi na wawili; 10ya tatu Zakuri, wanawe na nduguze, kumi na wawili; 11ya nne Seri, wanawe na nduguze, kumi na wawili; 12ya tano Nethania, wanawe na nduguze, kumi na wawili; 13ya sita Bukia, wanawe na nduguze, kumi na wawili; 14ya saba Asharela, wanawe na nduguze, kumi na wawili; 15ya nane Yeshaya, wanawe na nduguze, kumi na wawili; 16ya kenda Matania wanawe na nduguze, kumi na wawili; 17ya kumi Shimei, wanawe na nduguze, kumi na wawili; 18ya kumi na moja Uzieli, wanawe na nduguze, kumi na wawili; 19ya kumi na mbili Hashabia, wanawe na nduguze, kumi na wawili; 20ya kumi na tatu Shebueli, wanawe na nduguze, kumi na wawili; 21ya kumi na nne Matithia, wanawe na nduguze, kumi na wawili; 22ya kumi na tano Yeremothi, wanawe na nduguze, kumi na wawili; 23ya kumi na sita Hanania, wanawe na nduguze, kumi na wawili; 24ya kumi na saba Yoshbekasha, wanawe na nduguze, kumi na wawili; 25ya kumi na nane Hanani, wanawe na nduguze, kumi na wawili; 26ya kumi na kenda Malothi, wanawe na nduguze, kumi na wawili; 27ya ishirini Eliatha, wanawe na nduguze, kumi na wawili; 28ya ishirini na moja Hothiri, wanawe na nduguze, kumi na wawili; 29ya ishirini na mbili Gidalti, wanawe na nduguze, kumi na wawili; 30ya ishirini na tatu Mahaziothi, wanawe na nduguze, kumi na wawili; 31#Ufu 4:4; 5:8; 11:16ya ishirini na nne Romanti-ezeri, wanawe na nduguze, kumi na wawili.

Currently Selected:

1 Nya 25: SUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in