YouVersion Logo
Search Icon

1 Nya 24

24
Mgawanyo wa Makuhani
1 # Kut 6:23; Law 10:1; Hes 3:2; 26:60 Na zamu za wana wa Haruni ni hizi. Wana wa Haruni; Nadabu, na Abihu, na Eleazari, na Ithamari. 2#Hes 3:4; 26:61Lakini hao Nadabu na Abihu walikufa kabla ya baba yao, wala hawakuwa na watoto; kwa hiyo Eleazari na Ithamari wakafanya ukuhani. 3Akawagawanya Daudi, na Sadoki wa wana wa Eleazari, na Ahimeleki wa wana wa Ithamari, katika utumishi kwa kadiri ya usimamizi wao. 4Wakaonekana wakuu wengi wa wana wa Eleazari kuliko wa wana wa Ithamari; wakagawanyika hivi; wa wana wa Eleazari kulikuwa na kumi na sita, waliokuwa wakuu wa mbari za baba zao; na wa wana wa Ithamari, sawasawa na mbari za baba zao, wanane. 5#Yos 18:10; Mit 16:33; 18:18; Mdo 1:26Ndivyo walivyogawanyika kwa kura, wao kwa wao; kwani kulikuwa na wakuu wa patakatifu, na wakuu wa Mungu, wa wana wa Eleazari, na wa wana wa Ithamari pia. 6#1 Fal 4:3; Neh 8:4Naye Shemaya, mwana wa Nethaneli, mwandishi, aliyekuwa wa Walawi, akawaandika mbele ya mfalme, na mbele ya wakuu, na Sadoki kuhani, na Ahimeleki, mwana wa Abiathari, na wakuu wa mbari za baba za makuhani, na za Walawi; ikatwaliwa ya Eleazari mbari moja ya baba, na moja ikatwaliwa ya Ithamari. 7#Ezr 2:36; Neh 7:39Kura ya kwanza ikamtokea Yehoiaribu, na ya pili Yedaya; 8#Ezr 10:21ya tatu Harimu, ya nne Seorimu; 9ya tano Malkia, ya sita Miyamini; 10#Neh 12:4,17; Lk 1:5ya saba Hakosi, ya nane Abia; 11ya kenda Yeshua, ya kumi Shekania; 12ya kumi na moja Eliashibu, ya kumi na mbili Yakimu; 13ya kumi na tatu Hupa, ya kumi na nne Yeshebeabu; 14ya kumi na tano Bilga, ya kumi na sita Imeri; 15ya kumi na saba Heziri, ya kumi na nane Hapisesi; 16ya kumi na kenda Pethahia, ya ishirini Ezekieli; 17ya ishirini na moja Yakini, ya ishirini na mbili Gamuli; 18ya ishirini na tatu Delaya, ya ishirini na nne Maazia. 19#Hes 4:49; 1 Nya 9:25; 2 Fal 5:7; Lk 1:8,23Huu ndio usimamizi wao katika huduma yao, waingie nyumbani mwa BWANA kwa kadiri ya agizo lao, kwa mkono wa Haruni baba yao, kama BWANA, Mungu wa Israeli, alivyomwamuru.
Walawi Wengineo
20 # 1 Nya 23:16 Na wa wana wa Lawi, waliosalia; wa wana wa Amramu, Shebueli; wa wana wa Shebueli, Yedeya. 21#1 Nya 23:17Wa Rehabia; wa wana wa Rehabia, Ishia mkuu wao. 22#1 Nya 23:15Wa Waishari, Shelomothi; wa wana wa Shelomothi, Yahathi. 23#1 Nya 15:9; 23:19Na wana wa Hebroni; Yeria mkuu wao, Amaria wa pili, Yahazieli wa tatu, Yekameamu wa nne. 24Wana wa Uzieli, Mika; wa wana wa Mika, Shamiri. 25Nduguye Mika, Ishia; wa wana wa Ishia, Zekaria. 26#Kut 6:19; 1 Nya 23:21; Hes 3:20,33Wana wa Merari; Mali na Mushi; wana wa Yaazia; Beno. 27Wana wa Merari; wa Yaazia; Beno, na Shohamu, na Zakuri, na Ibri. 28#1 Nya 23:22Wa Mali; Eleazari, asiyekuwa na wana. 29Wa Kishi; wana wa Kishi; Yerameeli. 30#1 Nya 23:23Na wana wa Mushi; Mali, na Ederi, na Yeremothi. Hao ndio wana wa Walawi, kwa kufuata mbari za baba zao. 31Hao nao wakatupiwa kura vile vile, kama ndugu zao wana wa Haruni, machoni pa Daudi mfalme, na Sadoki, na Ahimeleki, na wakuu wa mbari za baba za makuhani na za Walawi; mbari za baba za mkuu, vile vile kama za nduguye mdogo.

Currently Selected:

1 Nya 24: SUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in