1
Mhubiri 5:2
Swahili Revised Union Version
Usiseme maneno ya ujinga kwa kinywa chako, wala moyo wako usiwe na haraka kunena mbele za Mungu; kwa maana, Mungu yuko mbinguni, na wewe upo chini, Kwa hiyo maneno yako na yawe machache.
Compare
Explore Mhubiri 5:2
2
Mhubiri 5:19
Tena, kwa habari za kila mwanadamu, ambaye Mungu amempa mali na ukwasi, akamwezesha kula katika hizo, na kuipokea sehemu yake, na kuifurahia amali yake; hiyo ndiyo karama ya Mungu.
Explore Mhubiri 5:19
3
Mhubiri 5:10
Apendaye fedha hatashiba fedha, Wala apendaye wingi hatashiba nyongeza. Hayo pia ni ubatili.
Explore Mhubiri 5:10
4
Mhubiri 5:1
Jitunze mguu wako uendapo nyumbani kwa Mungu; Maana ni heri kukaribia ili usikie, Kuliko kutoa kafara ya wapumbavu; Ambao hawajui kuwa wafanya mabaya.
Explore Mhubiri 5:1
5
Mhubiri 5:4
Wewe ukimwekea Mungu nadhiri, usikawie kuiondoa; kwa kuwa yeye hawi radhi na wapumbavu; basi, uiondoe hiyo uliyoiweka nadhiri.
Explore Mhubiri 5:4
6
Mhubiri 5:5
Ni afadhali usiweke nadhiri, Kuliko kuiweka usiiondoe.
Explore Mhubiri 5:5
7
Mhubiri 5:12
Usingizi wake kibarua ni mtamu, awe amekula kidogo, au awe amekula kingi; lakini kushiba kwake tajiri hakumwachi kulala usingizi.
Explore Mhubiri 5:12
8
Mhubiri 5:15
Alivyotoka tumboni mwa mamaye, atakwenda tena tuputupu kama alivyokuja; asichume kitu chochote kwa ajili ya kazi yake, hata akichukue mkononi mwake.
Explore Mhubiri 5:15
Home
Bible
Plans
Videos