YouVersion 標識
搜索圖示

Mwanzo 10

10
Mataifa yaliyotokana na Nuhu
(1 Nyakati 1:5-23)
1Hivi ndivyo vizazi vya wana wa Nuhu, yaani Shemu, Hamu na Yafethi, ambao walizaa wana baada ya gharika.
Wazao wa Yafethi
2Wana wa Yafethi walikuwa:
Gomeri, Magogu, Madai, Yavani, Tubali, Mesheki na Tirasi.
3Wana wa Gomeri walikuwa:
Ashkenazi, Rifathi na Togarma.
4Wana wa Yavani walikuwa:
Al-Yasa, Tarshishi, Kitimu na Rodanimu. 5(Kutokana na hawa mataifa ya pwani yalienea katika nchi zao, kwa koo zao katika mataifa yao, kila moja kwa lugha yake.)
Wazao wa Hamu
6Wana wa Hamu walikuwa:
Kushi, Misri#10:6 yaani Misraimu, Putu na Kanaani.
7Wana wa Kushi walikuwa:
Seba, Havila, Sabta, Raama na Sabteka.
Wana wa Raama walikuwa:
Sheba na Dedani.
8Kushi akamzaa Nimrodi, ambaye alikua akawa shujaa mwenye nguvu duniani. 9Alikuwa mwindaji hodari mbele za Mwenyezi Mungu; Ndiyo maana watu husema, “Kama Nimrodi, mwindaji hodari mbele za Mwenyezi Mungu.” 10Vituo vya kwanza katika ufalme wake vilikuwa Babeli, Ereki, Akadi na Kalne, katika nchi ya Shinari. 11Kutoka nchi ile alienda Ashuru, ambako alijenga miji ya Ninawi, na Rehoboth-Iri, na Kala, 12na Reseni, mji ulio kati ya Ninawi na Kala; huo ndio mji mkubwa.
13Misri alikuwa baba wa:
Waludi, Waanami, Walehabi, Wanaftuhi, 14Wapathrusi, Wakasluhi (hao ndio asili ya Wafilisti), na Wakaftori.
15Kanaani alikuwa baba wa:
Sidoni mzaliwa wake wa kwanza, Hethi, 16Wayebusi, Waamori, Wagirgashi, 17Wahivi, Waarki, Wasini, 18Waarvadi, Wasemari na Wahamathi.
(Baadaye koo za Wakanaani zilitawanyika, 19na mipaka ya Kanaani ikaenea kutoka Sidoni kuelekea Gerari hadi Gaza, kisha kuelekea Sodoma, Gomora, Adma na Seboimu, hadi kufikia Lasha.)
20Hawa ni wana wa Hamu kwa koo zao na lugha zao, katika nchi zao na mataifa yao.
Wazao wa Shemu
21Shemu, ndugu mkubwa wa Yafethi, alizaa wana pia. Shemu alikuwa baba wa wana wote wa Eberi.
22Wana wa Shemu walikuwa:
Elamu, Ashuru, Arfaksadi, Ludi na Aramu.
23Wana wa Aramu walikuwa:
Usi, Huli, Getheri na Mashi#10:23 yaani Mesheki.
24Arfaksadi alikuwa baba wa Shela,
naye Shela akamzaa Eberi.
25Eberi akapata wana wawili:
Mmoja wao aliitwa Pelegi, kwa kuwa wakati wake dunia iligawanyika; nduguye aliitwa Yoktani.
26Yoktani alikuwa baba wa:
Almodadi, Shelefu, Hasarmawethi, Yera, 27Hadoramu, Uzali, Dikla, 28Obali, Abimaeli, Seba, 29Ofiri, Havila na Yobabu. Hawa wote walikuwa wana wa Yoktani.
30(Eneo waliloishi lilienea kutoka Mesha kuelekea Sefari, kwenye nchi ya vilima iliyo mashariki.)
31Hao ndio wana wa Shemu kwa koo zao na lugha zao, katika nchi zao na mataifa yao.
32Hizi ndizo koo za wana wa Nuhu, kufuatana na vizazi vyao, katika mataifa yao. Kutokana na hawa mataifa yalienea duniani kote baada ya gharika.

目前選定:

Mwanzo 10: ONMM

醒目顯示

分享

複製

None

想要在所有設備上保存你的醒目顯示嗎? 註冊或登入