Mattayo MT. 11
11
1IKAWA Yesu alijiokwisha kuwaagiza wanafunzi wake thenashara, akatoka huka kwenda kufundisha na kukhubiri katika miji yao.
2Nae Yohana aliposikia huko gerezani matendo yake Kristo, alituma wawili katika wanafunzi wake, kumwambia, 3Wewe ndiye ajae, au tumtazamie mwingine? 4Yesu akajibu akawaambia, Enendeni mkamweleze Yohana mnayoyasikia na kuyaona: 5vipofu wanapata kuona, viwete wanatembea, wenye ukoma wanatakasika, viziwi wanasikia, wafu wanafufuliwa, na maskini wanakhubiriwa khabari njema. 6Na yu kheri ye yote asiyechukiwa nami. 7Nao wakienda zao, Yesu akaanza kuwaambia makutano khabari za Yohana, Mlitoka kwenda jangwani kutazama nini? Unyasi ukilikiswa na upepo? 8Lakini mlitoka kwenda kuona nini? Mtu aliyevikwa mavazi meroro? Watu wavaao mavazi meroro, wamo katika nyumba za wafalme. 9Lakini mlikwenda kuona nini? Nabii? Naam, nawaambieni, na aliye zaidi ya nabii. 10Kwa maana huyo ndiye aliyeandikiwa,
Tazama, mimi namtuma mjumbe wangu mbele ya uso wako.
Atakaeitengeneza njia yako mbele yako.
11Amin, nawaambieni, Hajaondokea mtu katika wazao wa wanawake aliye mkuu kuliko Yohana Mbatizaji: illakini aliye mdogo katika ufalme wa mbinguni ni mkuu kuliko yeye. 12Tangu siku za Yohana Mbatizaji hatta leo ufalme wa mbinguni hupatikana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka. 13Kwa maana manabii wote na torati walitabiri mpaka wakati wa Yohana. 14Na ikiwa mantaka kukubali, yeye ndiye Elia atakaekuja. 15Mwenye masikio ya kusikilia, na asikie. 16Nitafananisha na nini kizazi hiki? Kimefanana na watoto wakikaa sokoni, wanaowaita wenzao, 17wakinena, Twaliwapigia filimbi, wala hamkucheza; twaliomboleza, wala hamkulia. 18Maana Yohana alikuja, hali wala hanywi, wakanena. Yuna pepo. 19Mwana wa Adamu alikuja, akila na kunywa, wakanena, Mlafi huyu, na mnywa mvinyo, rafiki wa watoza ushuru na wenye dhambi! Na hekima imepewa haki na watoto wake.
20Ndipo akaanza kuikemea miji ile ambamo ilifanyika miujiza yake iliyo mingi, kwa sababu haikutubu. 21Ole wako, Korazin! Ole wako, Bethsaida! Kwa maana kama miujiza iliyofanyika kwenu ingalifanyika katika Turo na Sidon, wangalitubu zamani kwa kuvaa gunia na majivu. 22Lakini, nawaambieni, itakuwa rakhisi Turo na Sidon istahimili adhabu zao siku ya hukumu kuliko ninyi. 23Nawe Kapernaum, uliyeinuliwa hatta mbinguni, utashushwa hatta kuzimu: kwa maana kama miujiza iliyofanyika kwako, ingalifanyika katika Sodom, ungalikuwapo hatta leo. 24Lakini nawaambieni, itakuwa rakhisi inchi ya Sodom istahimili adhabu yake siku ya hukumu kuliko wewe.
25Wakati ule Yesu akajibu akasema, Nakushukuru, Baba, Bwana wa mbingu na inchi, kwa kuwa uliwaficha haya wenye hekima na busara, ukawafunulia wadogo: 26Naam, Baba, kwa kuwa ndivyo ilivyopendeza mbele yako. 27Nimekabidhiwa vyote na Baba yangu: wala hakuna mtu amjuae Mwana, illa Baba; wala hakuna mtu amjuae Baba illa Mwana, na ye yote ambae Mwana apenda kumfunulia. 28Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye mizigo nami nitawapumzisha. 29Jitieni nira yangu, jifunzeni kwa mfano wangu; kwa kuwa mimi ni mpole na moyo wangu umenyenyekea: nanyi mtapata raha rohoni mwenu; 30kwa maana nira yangu laini, na mzigo wangu mwepesi.
Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.