Yohana Utangulizi
Utangulizi
Injili ya Yohana iliandikwa na Mtume Yohana miaka mingi baada ya kufa na kufufuka kwa Isa Al-Masihi kwa kusudi la wote waisomapo waweze kumwamini Al-Masihi, na hivyo kuwa na uzima kupitia jina lake (20:31). Yohana anaanzia na dibaji ya kipekee iliyo katika Injili hii pekee, ambapo maisha ya Isa na Mungu Baba Mwenyezi kabla ya kutokea kwake yanaonyesha kwamba Isa hakuwa tu mtu mashuhuri, lakini alikuwa wa asili ya Mwenyezi Mungu. Miujiza ya Isa na mafundisho yake mengi ambayo hayajanakiliwa sehemu nyingine yoyote yameelezewa. Sehemu ndefu (14–17) inaelezea mafundisho ya Isa kwa mitume wake kabla ya kifo chake. Sehemu maalum inapewa kueleza kujitokeza kwa Isa kwa mitume wake baada ya kufufuka kwake.
Wazo Kuu
Injili ya Yohana inatilia mkazo wa hali ya uungu wa Al-Masihi kuliko Injili ingine yoyote, na kutupa ufafanuzi wa maisha yake. Ameelezewa kitamathali kama mwangaza, ukweli, upendo, mchungaji mwema, mlango, ufufuo na uzima, maji yaliyo hai, mkate wa kweli, na mengine mengi. Maandishi ya kusisimua katika sura 14–17 yanaonyesha upendo mkuu wa Isa kwa muumini, na amani itokayo katika kumtumaini Al-Masihi.
Mwandishi
Mtume Yohana.
Mahali
Efeso.
Tarehe
Kama mwaka wa 90–96 BK.
Mgawanyo
Dibaji kunyesha hali ya uungu wa Isa (1:1-14)
Huduma ya Isa kabla ya kwenda Galilaya (1:15–4:54)
Huduma ya Isa huko Galilaya, na upinzani uliomkabili huko Yerusalemu (5:1–10:42)
Kufufuliwa kutoka wafu kwa Lazaro (11:1-57)
Kukamilishwa kwa huduma ya Isa (12:1–13:38)
Mafundisho ya mwisho ya Isa (14:1–17:26)
Kufa na kufufuka kwa Isa (18:1–20:10)
Kuonekana kwa Isa baada ya kufufuka (20:11–21:25).
Neno: Maandiko Matakatifu™ NMM™
Hakimiliki © 2018 na Biblica, Inc.
Imetumiwa kwa ruhusa.
Haki zote zimehifadhiwa duniani kote.
Kiswahili Contemporary Scriptures™
Copyright © 2018 by Biblica, Inc.
Used with permission.
All rights reserved worldwide.