YouVersion 標誌
搜尋圖標

Mwa 7

7
Gharika Kuu
1 # Zab 91:1-10; Ebr 11:7; 1 Pet 3:20; 2 Pet 2:5,9; Mwa 6:9; Zab 33:18,19 BWANA akamwambia Nuhu, Ingia wewe na jamaa yako yote katika safina; kwa maana nimekuona wewe u mwenye haki mbele zangu katika kizazi hiki. 2#Law 11:1-31Katika wanyama wote walio safi ujitwalie saba saba, mume na mke; na katika wanyama wasio safi wawili wawili, mume na mke. 3Tena katika ndege wa angani saba saba, mume na mke; ili kuhifadhi hai mbegu juu ya uso wa nchi yote. 4#Ayu 22:16; 2 Pet 2:5Kwa maana baada ya siku saba nitainyeshea dunia mvua, siku arobaini mchana na usiku; na kila kilicho hai nilichokifanya juu ya uso wa nchi nitakifutilia mbali. 5#Mwa 6:22; Zab 119:6Nuhu akafanya kama vile BWANA alivyomwamuru.
6Naye Nuhu alikuwa mtu wa miaka mia sita hapo hiyo gharika ya maji ilipokuwa juu ya nchi. 7#Mt 24:38-39; Lk 17:27; Ebr 6:18Nuhu akaingia katika safina, yeye, na wanawe, na mkewe, na wake za wanawe pamoja naye; kwa sababu ya maji ya gharika. 8Na katika wanyama walio safi, na wanyama wasio safi, na ndege, navyo vyote vitambaavyo juu ya nchi, 9wakaingia katika safina alimo Nuhu, wawili wawili, mume na mke, kama vile Mungu alivyomwamuru Nuhu. 10Ikawa baada ya siku hizo saba, maji ya gharika yakawa juu ya nchi. 11#2 Pet 3:6; Mwa 8:2; Mit 8:28; Eze 20:19; Zab 78:23; Isa 24:18; Mal 3:10Katika mwaka wa mia sita wa maisha ya Nuhu, mwezi wa pili, siku ya kumi na saba ya mwezi, siku ile chemchemi zote za vilindi vikuu zilibubujika kwa nguvu, madirisha ya mbinguni yakafunguka. 12Mvua ikanyesha juu ya nchi, siku arobaini mchana na usiku. 13Siku ile ile Nuhu akaingia katika safina, yeye, na Shemu na Hamu na Yafethi, wana wa Nuhu, na mkewe Nuhu, na wake watatu wa wanawe pamoja naye; 14wao na kila mnyama wa mwitu kwa jinsi yake, na kila mnyama wa kufugwa kwa jinsi yake, na kila kitambaacho, chenye kutambaa juu ya nchi, kwa jinsi yake, na kirukacho kwa jinsi yake, kila ndege wa namna yo yote. 15Waliingia katika safina alimo Nuhu, wawili wawili, wa kila chenye mwili kilicho na pumzi ya uhai ndani yake. 16#Zab 91:1-16; 17:8; 145:20; 1 Pet 1:5Na walioingia, waliingia mume na mke, wa kila kitu chenye mwili, kama vile alivyomwamuru Mungu; BWANA akamfungia.
17Ile gharika ilikuwako juu ya nchi siku arobaini; nayo maji yakazidi, yakaieleza safina, ikaelea juu ya nchi. 18#Zab 104:26Maji yakapata nguvu, yakazidi sana juu ya nchi; na ile safina ikaelea juu ya uso wa maji. 19#Zab 104:6Maji yakapata nguvu sana sana juu ya nchi; na milima mirefu yote iliyokuwako chini ya mbingu ikafunikizwa. 20Maji yakapata nguvu, hata ikafunikwa milima kiasi cha mikono kumi na mitano. 21#Mwa 6:13,17; Ayu 22:16; Mt 24:39; Lk 17:27; 2 Pet 3:6Wakafa wote wenye mwili waendao juu ya nchi, na ndege, na wanyama wa kufugwa, na kila mnyama wa mwitu, na kila kitambaacho chenye kutambaa juu ya nchi, na kila mwanadamu; 22#Mwa 2:7kila kitu chenye pumzi ya roho ya uhai puani mwake kikafa, kila kilichokuwako katika nchi kavu. 23#Eze 14:14; Mal 3:17,18; Ebr 11:17; 1 Pet 3:20; 2 Pet 2:5Kila kilicho hai juu ya uso wa nchi kikafutiliwa mbali tangu mwanadamu hata mnyama wa kufugwa, na kitambaacho, na ndege wa angani; vilifutiliwa mbali katika nchi, akabaki Nuhu tu, na hao walio pamoja naye katika safina. 24#Mwa 8:3,4Maji yakapata nguvu juu ya nchi siku mia na hamsini.

目前選定:

Mwa 7: SUV

醒目顯示

分享

複製

None

想在你所有裝置上儲存你的醒目顯示?註冊帳戶或登入