1
Mk 13:13
Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia
Nanyi mtakuwa mkichukiwa na watu wote kwa ajili ya jina langu; lakini mwenye kusaburi hata mwisho, ndiye atakayeokoka.
對照
Mk 13:13 探索
2
Mk 13:33
Angalieni, kesheni, [ombeni], kwa kuwa hamjui wakati ule utakapokuwapo.
Mk 13:33 探索
3
Mk 13:11
Na watakapowachukua ninyi, na kuwasaliti, msitafakari kwanza mtakayosema, lakini lo lote mtakalopewa saa ile, lisemeni; kwa maana si ninyi msemao, bali ni Roho Mtakatifu.
Mk 13:11 探索
4
Mk 13:31
Mbingu na nchi zitapita; lakini maneno yangu hayatapita kamwe.
Mk 13:31 探索
5
Mk 13:32
Walakini habari ya siku ile na saa ile hakuna aijuaye, hata malaika walio mbinguni, wala Mwana, ila Baba.
Mk 13:32 探索
6
Mk 13:7
Nanyi mtakaposikia habari za vita na uvumi wa vita, msitishwe; hayo hayana budi kutukia, lakini ule mwisho bado.
Mk 13:7 探索
7
Mk 13:35-37
Kesheni basi, kwa maana hamjui ajapo bwana wa nyumba, kwamba ni jioni, au kwamba ni usiku wa manane, au awikapo jimbi, au asubuhi; asije akawasili ghafula akawakuta mmelala. Na hilo niwaambialo ninyi, nawaambia wote, Kesheni.
Mk 13:35-37 探索
8
Mk 13:8
Kwa maana taifa litaondoka kupigana na taifa, na ufalme kupigana na ufalme; kutakuwa na matetemeko ya nchi mahali mahali; kutakuwako na njaa; hayo ndiyo mwanzo wa utungu.
Mk 13:8 探索
9
Mk 13:10
Na sharti Injili ihubiriwe kwanza katika mataifa yote.
Mk 13:10 探索
10
Mk 13:6
Wengi watakuja kwa jina langu, wakisema, Mimi ndiye, nao watadanganya wengi.
Mk 13:6 探索
11
Mk 13:9
Nanyi jihadharini nafsi zenu; maana watawapeleka ninyi mabarazani; na katika masinagogi mtapigwa; nanyi mtachukuliwa mbele ya maliwali na wafalme kwa ajili yangu, kuwa ushuhuda kwao.
Mk 13:9 探索
12
Mk 13:22
kwa maana wataondoka Makristo wa uongo, na manabii wa uongo, watatoa ishara na maajabu, wapate kuwadanganya, kama yamkini, hata hao wateule.
Mk 13:22 探索
13
Mk 13:24-25
Lakini siku zile, baada ya dhiki hiyo, jua litatiwa giza, na mwezi hatautoa mwanga wake. na nyota za mbinguni zitakuwa zikianguka, na nguvu zilizo mbinguni zitatikisika.
Mk 13:24-25 探索
主頁
聖經
計劃
影片